Winga matata wa Manchester United, Amad Diallo, amethibitisha kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Hii ni baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mazoezi.
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi jioni, Diallo alieleza masikitiko yake kwa kuumia katika kipindi muhimu cha msimu, lakini akaahidi kurejea akiwa na nguvu zaidi.
"Ninasikitika sana kuandika ujumbe huu katika kipindi muhimu cha msimu. Kwa bahati mbaya, nitakuwa nje kwa muda kutokana na jeraha,” Diallo aliandika kwenye X.
”Nitarudi nikiwa na nguvu zaidi!! Ni wakati wa kuwaunga mkono wachezaji wenzangu kutoka nje ya uwanja. Bado kuna mengi ya kupigania," aliongeza.
Enjoying this article?
Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
Jeraha hili linakuja wakati ambapo Manchester United inakabiliwa na orodha ndefu ya wachezaji waliojeruhiwa.
Mbali na Diallo, wachezaji wengine muhimu kama Manuel Ugarte, Toby Collyer, na Kobbie Mainoo pia wanakabiliwa na majeraha, hali inayomlazimu kocha Ruben Amorim kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake.
Kutokana na hali hii, Amorim amewaita wachezaji kadhaa kutoka akademi ya vijana ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na majeruhi.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Chido Obi, Sekou Kone, na Harry Amass, ambao wanatarajiwa kutoa mchango muhimu katika mechi zijazo.
Amad Diallo, mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Manchester United mnamo Januari 2021 kutoka Atalanta.
Mchezaji huyu mwenye asili ya Ivory Coast amekuwa na msimu mzuri, akifunga mabao tisa na kutoa pasi saba za mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
Hata hivyo, jeraha hili linamaanisha kuwa hatoweza kuongeza takwimu hizo kwa sasa.
Kutokuwepo kwa Diallo na wachezaji wengine muhimu kunaleta changamoto kubwa kwa Manchester United, hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mashabiki na wachambuzi wa soka wana wasiwasi kuhusu uwezo wa kikosi kilichosalia kukabiliana na mechi zijazo, hasa dhidi ya timu zenye ushindani mkali.
Hata hivyo, kocha Amorim ana matumaini kwamba wachezaji vijana watajitokeza na kutoa mchango muhimu katika kipindi hiki kigumu.
Mashabiki na wachezaji wenzake wanamtakia Diallo ahueni ya haraka, wakisubiri kwa hamu kurejea kwake uwanjani msimu ujao.
Kwa sasa, Manchester United inajiandaa kwa mechi zijazo za Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwemo dhidi ya Tottenham Hotspur leo, Februari 16, 2025, saa moja unusujioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!