Kenya Power logo

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Februari 16.

 

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

 

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja unusu  jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Uasin Gishu, Kiambu, na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kileleshwa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Sehemu za maeneo ya Jua Kali, na Simba Cement katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kihunguru, Rainbow na NKG katika kaunti ya Kiambu pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Malindi Complex, Malindi Police, na Golf pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.