Thika Road.

Mamlaka ya Barabara Kuu ya Kenya (KeNHA) imetangaza kufungwa kwa muda kwa sehemu ya barabara ya Thika Superhighway katika eneo la Juja Highpoint, maarufu kama Centurion.

 

Kulingana na taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa KeNHA, Eng. Kung’u Ndungu, barabara hiyo itafungwa kwa siku nne kuanzia Jumamosi, Februari 15, 2025, hadi Jumanne, Februari 18, 2025, kati ya saa tano usiku na saa kumi na mbili asubuhi.

 

Hatua hii imechukuliwa ili kuruhusu ujenzi wa daraja jipya la watembea kwa miguu.

 

Madereva wanaoelekea Nairobi wametakiwa kutumia barabara ya mzunguko iliyo nyuma ya kituo cha mafuta cha Lex Petrol kabla ya kuungana tena na Thika Superhighway.

 

Vilevile, wale wanaoelekea Thika watatumia mzunguko ulio nyuma ya Hoteli ya Centurion kabla ya kuungana tena na barabara kuu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 

KeNHA imetoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapopita karibu na eneo la ujenzi, kufuata mpango wa usimamizi wa trafiki uliopendekezwa.

 

Watumizi wa barabara pia wametakiwa kushirikiana na maafisa wa trafiki na maaskari wa usalama barabarani walioko eneo husika ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa utaratibu.