
Rais wa Liberia awasimamisha kazi wafanyakazi wa serikali 450
Rais wa Liberia Joseph Boakai aliwafurusha wafanyakazi wake wa serikali 450 kwa tuhuma za kususia kuelezea walikopata mali zao.
Rais Boakai alichukuwa hatua hiyo baada ya wafanyakazi hao kushindwa kuelezea walikopata mali zao kwa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini humo.
‘Hawatakuwa kazini kwa mwezi mmoja labda waeleze walikopata mali zao kwa tume ya kupambana na ufisadi (LACC) vizuri’’Rais Boakai alisema.
Rais alisema kuwa viongozi hao walikiuka madili ya kazi kwa kutoeleza ni wapi walikotoa mali zao kwa njia ya wazi na ya ustaarabu bila kubabaika.Rais alikuwa ameapa kupigana na ufisadi wakati ambapo alichukua hatamu za uongozi.
Hata hivyo alisema kuwa kwa viongozi hao kususia kueleza ni wapi walikotoa mali zao ni kulemaza juhudi zake za kupambana na ufisadi akisema kuwa ni ahadi na kiapo alichokila kwa ajili ya kulinda mali za raia hivyo ni wajibu wake kama rais kutekeleza yafaayo .
Baaadhi ya viongozi waliotimuliwa ni Waziri wa elimu,Waziri wa afia,wafanyakazi maalum wa sekta ya utali na uekezaji vilevile rais aliwasimamisha kazi viongozi wa ngazi za juu wa kaunti ambao aliwaweka katika orodha kubwa ya wafanyakazi fisadi.
Tume ya kupambana na ufisadi nchini Liberia (LACC) ilitoa orodha ya majina ya jumla ya watu 457 waliotajwa kama viongozi serikalini katika viwango tofauti tofauti ambao ni fisadi.
Itakumbukwa wazi kuwa mnano Julai mwaka Jana Rais Boakai alitangaza kupunguzwa kwa mshahara wake kwa asilimia 40 kama njia moja wapo ya kupambana na ufisadi na kuhakikisha kuwa analiweka taifa lake katika hali nzur kiuchumi Pamoja na raia wake kuishi vyema.
Rais aliyemtangulia Bwana George Weah alituhumiwa na wengi kwa utumizi mbaya wa mamlaka na afisi vilevile walimkashifu kwa kuwa fisadi, kuporomosha Uchumi wa nchi na kufanya maisha ya raia kuwa magumu zaidi.
Hata hivyo uamuzi wara rais Boakai umeshutumiwa na wengi wakisema kuwa kuwasimamisha kazi wafanyakazi kwa mwezi mmoja hilo ni swala la kujinasua tu mbele ya macho ya umma ionekane yuafanya kazi ila ni hatua hafifu sana na haifai kamwe.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!