Msani wa filamu Irene Uwoya ameweka wazi kwamba yuko tarari kufunga ndoa na mwanaume yeyote mwaka huu wala habaguwi.

Jambo ambalo amesisitiza na kupendelea ni kwamba akipata mtumishi wa Mungu atafurahia sana

" Mimi natamani kuoleka sana mwaka huu, napendekeza mwanaume ambaye anamujua Mungu, mtumishi wa Mungu lakini bado sichagui. alisema muigizaji huyo

Hata wewe ukitaka kunioa sitakata nitakubali, " alimwambia aliyekuwa akimuuliza maswali, baada ya kumutania kwamba "unataka mtumishi wa Mungu kama mimi"

Irene Pancras Uwoya  alizaliwa mwaka 1988 ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu na video  na mjasiriamali ambaye ni mfanyi biashara wa Tanzania,  anajulikana zaidi kwa jina lake la kazi Irene Uwoya na kwa jukumu lake la filamu Oprah. Alianza kazi yake ya kitaaluma mwaka 2007 pamoja na waigizaji wengine wa filamu za bongo kama vile Vincent Kigosi na Steven Kanumba.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 Safari yake ya ndoa haijakuwa na bahati vile kwani amewahi kujaribu ndoa mara kadha.

Mwaka 2008 Irene aliolewa na mchezaji wa mpira wa miguu wa Rwanda na nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda Hamad Ndikumana ambaye baadaye alifariki.

Mwaka 2011alijaribu tena ila wanandoa hao walikuwa na mtoto mmoja aitwaye Krish na miaka michache baadaye wanandoa hao walitengana.

Mwaka 2017 alifunga ndoa tena, safari hii kwa mwanamuziki wa bongo flava, Abdulaziz Chande maarufu kitaalamu kama Dogo Janja.

Baadhi ya kumbukumbu za mwigizaji huyu ni kwamb Mwaka 2006 aligombea katika shindano la 'Miss Tanzania Beauty Pageant' na kushika nafasi ya tano; Muigizaji mwenza Wema Sepetu alitawazwa kuwa Miss Tanzania mwaka 2006-2007 katika mapishano hayo.

Irene Uwoya ni sta maarufu nchini Tanzani na alianza kazi yake kama mwigizaji katika filamu za Bongo. Ameshirikishwa katika filamu zaidi ya 20 ndani na nje ya Tanzania.