Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atakutana na makamu wa rais wa Marekani JD Vance kwa mazungumzo mjini Munich baadae huku mazungumzo ya vita hivyo yakitarajiwa kutawala mkutano mkubwa wa usalama wa viongozi wa dunia.

Zelensky pia anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio.

Hayo yanajiri wakati Ukraine na washirika wake wa Ulaya wakiendelea kujibu tangazo la kushtukiza la Rais wa Marekani Donald Trump wiki hii kwamba yeye na Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana katika wito wa kuanza mazungumzo ya kumaliza vita hivyo.

Trump alisema Alhamisi kwamba anatarajia maafisa wa Urusi pia watakuwa katika mkutano huo mjini Munich na kupendekeza kuwa wanaweza kukutana na maafisa wa Marekani na Ukraine - lakini afisa wa ngazi ya juu wa Ukraine alisema mazungumzo na Urusi hayatarajiwi.

"Urusi itakuwepo pamoja na watu wetu na Ukraine pia inaalikwa, bila uhakika ni nani atakayekuwa huko kutoka nchi yoyote - lakini watu wa ngazi ya juu kutoka Urusi, kutoka Ukraine na kutoka Marekani." rais wa Marekani amesema katika matamshi yake kwa waandishi wa habari.

Rais Trump alizungumza na marais wote wawili wa hizo nchi zinazokabiliana kwanza na Putin wa Urusi, kisha Zelensky wa Ukrain.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Akielezea mazungumzo hayo kama "makubwa", Trump alisema kuna uwezekano mzuri wa kumaliza vita hivyo vya kutisha, vya umwagaji damu".

Lakini alitilia shaka uwezekano wa Kyiv kujiunga na muungano wa kijeshi wa Nato na pia "haiwezekani" kwamba Ukraine inaweza kurudi kwenye mipaka yake ya kabla ya uvamizi mnamo 2014.

Zelensky - kwa upande wake alisema kwamba "haipendezi sana" kwamba Trump alikuwa amezungumza na Putin kabla yake - alionya kuwa Ukraine haitakubali mpango wowote wa amani uliopendekezwa na Marekani na Urusi bila ushiriki wa Kyiv,

"Hatuwezi kukubali, kama nchi huru," alisema, akisisitiza kwamba kipaumbele chake ni "uhakika wa usalama", kitu ambacho hakukiona bila msaada wa Marekani.

Zelensky amesema washirika wa Ulaya "wanapaswa kuwa katika meza ya mazungumzo pia", huku kukiwa na hofu inayoongezeka kote barani humo kwamba hatua ya Trump kuanzisha mazungumzo na Putin kunaweza kusababisha makubaliano tofauti kati ya Marekani na Urusi kuhusu mustakabali wa Ukraine na Ulaya.Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumzia hili annesema kwamba ni Zelensky pekee anayeweza kufanya mazungumzo kwa niaba ya nchi yake na Urusi, akionya kuwa "amani ambayo ni utekaji" itakuwa "habari mbaya kwa kila mtu".