Bunge la seneti limemsimamisha seneta mteule Gloria Orwoba kutohudhuria vikao vya bunge hilo kwa muda wa siku 79

Hii ni baada ya kushutumiwa kwa utovu wa nidhamu kufuatia matamshi aliyotoa kuhusu afisa wa ngazi ya juu wa Seneti.

Seneta wa Meru Kathuri Murungi ambaye pia ni Naibu Spika wa Seneti, alitangaza kusitishwa kwake kufika kwenye bunge katika kikao cha jana Jumatano. .

"Baada ya kuzingatia suala hili na kuzingatia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu, Seneta Gloria Orwoba sasa amesimamishwa kuhudhuria vikao," Murungi alisema.

Murungi alifafanua zaidi kuwa siku 79 za kalenda Orwoba ilikusudiwa kutumika mnamo 2023 lakini haikuwa imeanza sasa itaanza Jumatano, Februari 12, 2025, mpaka kufikia Alhamisi, Mei 1, 2025

Seneta Orwoba alipopewa  fursa ya kuhutubia Baraza la seneti kabla ya kuondoka kuanza kutumikia likizo ya lazima, Orwoba aliomba radhi, akieleza kuwa haikuwa nia yake ya kudhihaki Seneti.

"Nashukuru kwa kunipa muda huu wa kuomba radhi kwa wajumbe wa Bunge hili na wafanyakazi ambao huenda niliwakosea. Kama nimemkosea mtu yeyote, natoa msamaha wangu wa dhati kutoka kwa  moyo wangu," alisema.

Seneta mteule Gloria Orwoba alishutumiwa kwa kutoa madai yasiyothibitishwa ya unyanyasaji wa kingono na ufisadi. Kamati ya Madaraka na Upendeleo "power and previleges" ya Seneti ilisema seneta huyo mwenye utata alikataa kufika mbele yake kujitetea. Maseneta hao kwa kura nyingi walipitisha ripoti ya kamati hiyo kumsimamisha seneta huyo wa UDA kwa miezi sita lakini baadaye siku zilipunguzwa na kufikia miezi mitatu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

. "Baada ya kumpa Seneta Gloria Orwoba fursa ya kusikilizwa, alikataa kushiriki katika uchunguzi na kamati ya mamlaka na upendeleo "power and previleges" na kwa hivyo kamati iliona kushikilia mashitaka. Kamati ilizingatia ushahidi ulio mbele yake juu ya shtaka hili, na kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote kinyume au kukanusha mashtaka, kwa hivyo mashtaka yalithibitishwa," kamati  iliongeza. 

Orwoba pia alishtakiwa kwa kutoa madai yasiyothibitishwa ya upendeleo, ubaguzi, na ufisadi katika kundi la Seneti la Whatsapp.

Senetor Orwoba aliteuliwa na chama tawala cha UDA kuwakilisha wanawake katika bunge la seneti.