
Usuli na safari ya msanii Dully Sykes
Abdul Sykes alimaarufu msanii Dully Sykes alizaliwa mnamo tarehe 4 Disemba,1980 Tanzania ni msanii wa haiba tena wa viwango vikubwa katika taasinia ya mziki wa bongo.
Dully Sykes ni mtoto wa Ebby Sykes,Dully anasawiriwa na wengi kama msanii mkongwe tena wa misimu katika ulingo wa mziki, yeye ndiye alikuwa mwasisi wa ukumbi wa Swahili na maziwa makuu Afrika(Swahili Dancehall and great lake Afrika).
Msanii Dully ndiye alikuwa mwanzilishi wa mziki aina ya Bongo flava na katika vibao vyake vya mwanzoni vilivyovuma na kutamba enzi zile ni kama Julieta,Salome,Historia ya kweli na Leah wakati huo akizindua albamu yake ya kwanza alioiita Historia ya Kweli mwaka 2003.
Dully mara nyingi alipopanda jukwani alishangiliwa na wengi huku mashabiki wake wakimpa sifa kedekede na kumfafananisha na kio cha jamii tena kama manukato yalionukia,mashabiki wake walichelea kumwita Dully na badala yake wakambandika jina la msimbo kama Mwanasesele kuashiria mfalme wa vibao vya kuvunja watu mbavu.
Msanii Dully kando na kuimba pia ana uwezo wa kuandika nyimbo katika viwango tofauti katika misimu tofauti na kwa wakati stahiki,aliwahi kurekodi miziki yake katika studio ya Dhahabu rekodi zama za kale.
Dully ni mmoja wa wasanii wa bongo ambao kwa miongo kadhaa wamevumilia na kushinda mawimbi na mikengeuko ya miziki na ujio wa masuala ya teknolojia na mitandao ya akili unde.
Aidha msanii Dully aliwahi kuwashirikisha na kuwakaribisha wasanii wengine wa haiba kimziki kama Mario na Shetta ambao aliwataja kama viungo muhimu katika utunzi na uimbaji wao kimtindo.
Msanii Dully ni mwanamziki aliye na historia pana na heshima zake, huwa anafahamu na kuuchukulia mziki kama sana yoyote ile ifikapo wakati wa kuimba au kuandika yeye hufanya kwa ustadi wa hali ya juu.
Kibao kipya ambacho msanii Dully amekiimba wakishirikiana na msanii Alikiba kinaitwa Zali kibao ambacho kiko na miezi miwili kikiwa kwa soko ila kimewavutia sana mashabiki Pamoja na wapenzi wa aina ya mziki wa Bongo katika mitandao ya Kijamii kule Youtube, Instagram na Tiktok zaidi ya mashabiki elifu tano.
Dully Sykes anazidi kuwaonyesha wasanii chipukizi Pamoja na mashabiki wake kuwa sanaa ya mziki haihitaji pupa,bezo wala ushindani wa wivu bali ni kucharaza kazi safi kisha unasubiri mashabiki wanaamue na wanakuweka kwenye mizani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!