KPLC staff

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 12, 2025.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, West Pokot, Kakamega, Tharaka Nithi, Kitui, na Kwale.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Westlands Kawangware, na Umoja 2 zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Sigor na Kainuk katika kaunti ya West Pokot yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Shule ya msingi ya Lurambi katika kaunti ya Kakamega pia itakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Tharaka Nithi, maeneo ya Kathwana na Matiri yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Maeneo ya Wikililye, Ikanga, na Mbitini katika kaunti ya Kitui yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu za maeneo ya Tiwi na Kombani katika kaunti ya Kwale pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.