
Sakaja aongoza zoezi la usafi jijini Nairobi
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja aliweka jiji kuu la Nairobi katika sura mpwa kama kile kilichoonekana kama kuleta mwamko mpya wa utendakazi.
Gavana Sakaja kupitia kwa halimashauri ya jiji la Nairobi aliwatangazia wafanyabiashara,wachuuzi na wamiliki wa nyumba mabadiliko ambayo yalipaswa kutekelezwa Katikati ya jiji la Nairobi kwa kipindi maalum ili wayafahmu .
Halimashauri ya Jiji la Nairobi(Nairobi city council )ilitoa arifa kwa wachuuzi wote walio Katikati ya jii kuhiari kuondoka ili kuipa nafasi halimashauri hiyo kufanya usafi na kuweka mipango maalum ya kukarabati na kuondoa mabango ya matangazo ya biashara katika sehemu za umma.
Mpango huo ulipozinduliwa na kuwaamuru wachuuzi wote kuondoka Katikati ya jiji la Nairobi wengi walionekana kupinga na kuutaja uamuzi huo kama wa dharura na kudai kuwa kama muungano wa wachuuzi jijini Nairobi hawakushauriwa kabla ya uamuzi huo kuafikiwa.
Halimashauri ya jii la Nairobi ilikuwa imetangaza kuwa Wachuuzi,wamiliki wa majumba na wafanyabishara ambao walio na mabango yanayoning’inia katika Barabara za wasafiri wa miguu kuondoa mabango hayo ya biashara.
Na kuwapa muda wa Miezi mitatu wamiliki wote wa majumba Katikati ya jiji la Nairobi kuyapaka rangi ili kulifanya jiji liwe safi na la kuvutia.
Baada ya uamuzi huo kutolewa na usimamizi husika Katikati ya jiji kuu la Nairobi mazingira yalibadilika na kuonekana kuwa ya kuvutia jambo ambalo lilisababisha kukosekana kwa mrundikano wa taka Katikati ya jiji huku watu walionekana kupishana kwa wepesi kutokana na utaratibu wa kupita bila kugongana.
Kutokana na juhudi hizo za kusafisha maeneo ya Katikati ya jiji kuu la Nairobi Gavana Sakaja mnamo Februari 11,2025 aliandaa mkutano kuwahutubia wachuuzi na wafanyabiashara ambao ni walemavu alipowahimiza kutotishika na shughuli ya kuwaondoa wachuuzi Katikati ya jiji la Nairobi.
Katika usemi wake Gavana alisema kuwa hamna mtu yeyeto alikuwa analengwa kufukuzwa bali ni mipango wa serikali ya Nairobi kuweka usafi na mipangilio Madhubuti.
‘’Hamna yeyeto anayekuzuia kufanya biashara ila kuna njia maalum ambayo tutafuata ili kuendesha biashara zetu kuna sehemu kama kaunti hatukubali biashara kutendeka ila tutaweka mikakati maalum ili biashara zenu ziendelee’’. Gavana alisema.
Sakaja alimuamuru mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko Bi Jane Wangui kuandaa mkutano na wafanyabishra,wachuuzi na washikadau katika sekta hii ili kuwe na utaratibu wa kuendesha biashara. Bwana Sakaja aliwatunuku walemavu vitimaguru(wheelchairs) kutoka kwa serikali ya Kaunti ya Nairobi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!