
Ni kikao ambacho kilirejelea vikao vyake siku ya Jumanne 11 Februari,2025 baada ya kuwa kwenye likizo ya miezi miwili.
Wabunge walirejelea vikao vyao baada ya mahakama kuu kutoa uamuzi uliobatilisha uamuzi wa Sipika wa Bunge la taifa Moses Masika Wetang’ula ambaye katika uamuzi wake mwaka wa 2022 alikuwa ametangaza kuwa mrengo wa Kenya kwanza ndio uliokuwa na idadi kubwa bungeni.
Baada ya uchaguzi huo kutamatika spika Wetangula alitangaza kuwa Kenya Kwanza walikuwa na wabunge 179 na azimio walikuwa na wabunge 157 kuashiria kuwa Kenya kwanza ndio waliokuwa wengi katika bunge la taifa.
Ila katika idadi ya mwanzoni azimio walikuwa na idadi ya wabunge 171 na Kenya kwanza walikuwa na 157 kuashiria kuwa Azimio ndio walikuwa na idadi kubwa bungeni kulingana na mjibu wa sheria na uchaguzi uliofanywa.
Baada ya pingamizi za hapa na pale Azimio waliwasilisha kesi kortini kutaka ufafanuzi wa kutaka kujua ni pande gani ya mrengo ambayo ilikuwa na idadi ya wabunge wengi bungeni.
Lakini katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu walioamua kesi kwa kusema kuwa uamuzi wa Spika Wetangula wa kuutangaza mrengo wa Kenya Kwanza kama waliowengi bungeni alikiuka sheria na ilikuwa kinyume.
Hata hivyo vikao vya bunge viliporejelewa ilikuwa ni zamu ya sipika wa bunge la Taifa kutegua kitendawili hicho cha uamuzi wa mahakama kuhusu ufafanuzi wa ni mrengo gani uliokuwa na wabunge wengi na upi uliokuwa na wabunge wachache.
Kwa kuzingatia uamuzi wa korti aliyekuwa kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwa angelazimika kumpokeza virago kiongozi wa walio wachache bungeni bwana Junet Mohammed na kiranja wa walio wengi Sylivanus Osoro wajibu wake kupokelewa na Milly Odhiambo kulingana na uamuzi wa mahakama japo hilo swala liliachiwa wabunge kujadili kabla ya uamuzi kufanywa.
Kuna masuala mengi ambayo yalitendeka baada ya uamuzi wa Sipika kuamua na baadaye kamati mbalimbali ziliundwa na kuendesha shughuli za bunge kwa utaratibu bila wasiwasi wowote hata hivyo maamuzi ya mahakama ni lazima yaheshimiwe.
Kilichosubiriwa sasa ni kusikiliza mwelekeo wa Sipika na kuwahusisha wabunge ili uamuzi wa suala hilo la wengi na wachache bungeni liamuliwe na kila shughuli ziendelee kwa utaratibu
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!