Viongozi wamtakia kila la heri Raila katika kiti cha AUC

Baada ya siku moja kutamatika kwa hafla iliyoandaliwa Jumatatu Februari 10,2025 kwa ajili ya kumwombea Raila Odinga katika safari yake ya kuchaguliwa kama mwenyekiti wa AUC.

Viongozi mbali mbali walijitokeza kumhongera na kumtakia kila la heri katika uchaguzi huo ambao umeratibiwa kufanyika  siku ya Jumamosi Februari 15,2025.

Wakili Nelson Havi alidokeza kuwa kulingana na historia pana na uzalendo ambao bwana Odinga amekuwa nao kwa taifa letu la Kenya ikiwa Pamoja na tajiriba ya uongozi alimsawiri Odinga kama chaguo bora la Kenya na la Afrika kwa Jumla.

Seneta wa Nyandarua John Methu naye kwa upande mwingine alimtakia kiongozi wa ODM kila la heri katika uchaguzi huo ujao ila alipinga pendekezo la wabunge zaidi ya mia moja (100) ambao waliratibiwa kuandamana naye katika safari ya Addisababa kule Uhabeshi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kulingana na kauli za bwana Methu aliwazia kuwa wabunge zaidi ya 100 watakaofika Addisababa kwa hafla ya kushuhudia upigaji kura huo ukifanyika alionelea kuwa hiyo ilikuwa ni  kutumia ushuru wa wananchi vibaya na badala yake alipendekeza akisema kuwa bwana Odinga ana usimamizi wa uhazili wake  ambao unastahili kuwa umetenga bajeti kwa ushirikiano na kamati andalizi ya masula ya kigeni ili kufanikisha kila kitu bila kugusa pesa za mlipa ushuru.

Kwa upande mwingine naibu Sipika katika bunge la taifa bi Gladys Boss Shollei alimmiminia sifa bwana Odinga akimtaja kama mzalendo na mtu mwenye utu zaidi wa kupenda nchi yake kuliko maslahi yake alisema hayo akihojiwa na kituo kimoja cha runinga humu nchini.

Bi Sholei alikariri kuwa kulingana na historia ya Raila Odinga ya siasa yeye ndiye mtu ambaye anayafahamu masuala ambayo huwaathiri wananchi sana na pia anatajiriba pana katika uongozi.Alikuwa akieleza jinsi Raila alivyokuwa mhimili imara katika serikali za mwanzoni alitaja serikali ya Moi,Kibaki,Uhuru na Ruto.

Hata hivyo katika hotuba ya bwana Odinga siku ya Jumatatu kwa hafla ya maombi ya kumwombea, Odinga alisema yuko tayari kuongoza bara la afrika akikariri kuwa ana matumaini ya kuibuka  na ushindi.