
Wachezaji na wakufunzi wa timu ya Adana Demirspor waliondoka uwanjani wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi yao ya Ligi Kuu ya Uturuki katika uwanja wa Galatasaray Jumapili, Februari 9, wakipinga penalti ya kutatanisha iliyotolewa dhidi yao.
Viongozi wa ligi Galatasaray walichukua uongozi katika dakika ya 12 baada ya mchezaji wao mpya Alvaro Morata kufunga penalti iliyotolewa dhidi yao.
Lakini wakati mchezo ukiendelea, meneja wa Adana Demirspor Mustafa Alper Avcı aliwaita wachezaji wake kwa majadiliano mafupi.
Muda mfupi baada ya mkutano huo mfupi, timu nzima ya Adana Demirspor ilitoka nje ya uwanja na kuelekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
Refa naye pia aliondoka nje ya uwanja, na baadaye ikatangazwa kuwa mechi imesimamishwa.
Makamu wa rais wa Adana Demirspor Metin Korkmaz alisema uamuzi huo ulielekezwa kwa bodi ya waamuzi na sio Galatasaray.
Aliongeza kuwa uamuzi huo ulichukuliwa na rais Adana Demirspor Murat Sancak ambaye alionekana kwenye mahojiano ya televisheni siku ya Jumamosi na kusema, "Naamini mwamuzi anataka kuonekana mzuri kwa Galatasaray."
Baada ya mchezo huo Sancak alithibitisha uamuzi huo wa penalti ndiyo sababu ya kuwaamuru wachezaji waache mechi na kusisitiza kuwa hatua hiyo haina uhusiano wowote na Galatasaray.
"Tulikuwa 99% tutapoteza leo," aliongeza.
Shirikisho la Soka la Uturuki litatoa uamuzi wa mwisho kuhusu mechi hiyo.
"Sidhani kama huu ni uamuzi usio na hatia. Huu ni uharibifu mkubwa kwa soka ya Uturuki. Samahani. Kuna juhudi kila mara kufanya soka la Uturuki kuonekana mbaya," meneja wa Galatasaray Okan Buruk alisema baada ya mchezo huo.
Kisa kama hicho kilitokea msimu uliopita wakati Istanbulspor pia ilijiondoa uwanjani wakati wa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Trabzonspor.
Mwamuzi wa msimu uliopita Halil Umut Meler alipigwa ngumi na rais wa MKE Ankaragucu Faruk Koca mwishoni mwa mechi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!