Mshukiwa wa wizi wa Lori Ibrahim Hassan akamatwa.

Aliyekuwa mshukiwa mkuubwa wa wizi wa malori Ibrahim Hassan hatimaye alikamatwa na polisi baada ya mbinu zake za wizi kutibuka.

Ibrahim Hassan anaripotiwa kuwa ni mmoja wa miongoni mwa wezi sugu ambao wamekuwa wakiwahangaisha madereva katika Barabara kuu ya makutano kutoka Isiolo kuelekea Garibatula.

Ibrahimu Hassan alisimama barabarani kisha akaunyosha mkono wake ishara ya kulisimamisha lori ili apewe kambara lori nambari ya usajili  KCC 7235 lililokuwa kwenye  barabara kuu ya Isiolo Garibatula dereva wa lori hilo alikuwa na roho ya utu aliaazimia  kusimama kisha akambebe Hassan.

Katika usemi wao walikubaliana kuwa mwisho wa lifti ya Hassan ingeishia mji wa ARCHERS lakini walipofika mjini Hassan alisusia kushuka kisha akamwamuru dereva kuendelea na mwendo,dereva aliposusia Hassan alichomoa  kisu kisha akamtishia kumdunga.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya dereva kuona kisu aliijawa na hofu na kuruka nje ya lori hapo ndipo  Ibrahim alipata mwanya wa kutoroka na lori akiendesha kwa kasi dereva  aliponea kudungwa visu kwa kukimbilia usalama wake na kuenda kuripoti katika kituo cha polisi cha  Archers.

Ibrahim alipokuwa katika hali ya kutoroka kwa kuendesha gari kwa kasi hivo alipotoka katika Barabara kuu ya Isiolo Garibatula na kuingia katika Barabara ndogo ya matope aliendesha hilo lori kwa kasi ya kufa mtu .

Alipokuwa akiendesha lori hilo alishutuka akiwa ameelekea katika mlango wa kituo cha polisi cha Archers bila kufahamu kuwa Barabara hiyo ilikuwa ikielekea kituoni akazuumu kupiga kona kurudi upesi alikotoka  lakini wapi wasiwasi wake ulimshitaki hapo ndipo alipofuatwa na maafisa wa usalama unyo kwa unyo.

Kutokana na hali ya   kuendesha lile lori kwa kasi bila kuzingatia hali ya Barabara ibrahimu alishutukia kama amegonga mti kisha akasimama,maafisa wa polisi waliokuwa wamemfuta sako kwa bako walifanikiwa kumnasa.

Bwana Hassan alikamata na maafisa wa usalama waliomkuta akiwa na upanga,kisu na parafujo kwashiria kuwa alikuwa yuko tayari kutekeleza vitendo vya udaidi vikiwemo mauaji.

Kwa sasa Hassan yuko mbaroni ambapo kitengo cha kupambana na magaidi cha DCI kimemchukua ili akisaidie katika kufanya uchunguzi na kuwakamata wengine eneo  hilo la Isiolo limekuwa likiripotiwa kwa wizi wa malori na vifo mara kwa mara.