Athari za uamuzi wa korti katika muungano wa serikali ya Kenya kwanza bungeni
Baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa muungano wa Azimio ndio ulio na idadi nyingi ya wabunge, uamuzi huo utaonekana kuiweka serikali ya Kenya Kwanza katika hali ngumu ya na upitishaji wa miswada mbalimbali katika bunge la taifa.
Kulingana na tangazo la awali ambapo Spika wa bunge la taifa Moses Masika Wetang’ula alilotangaza katika bunge la taifa mnamo Oktoba 6,2022 alitangaza kuwa muungano wa Kenya kwanza ulikuwa na idadi kubwa ya wabunge 179 dhidi ya Azimio ambao walikuwa na wabunge 157.
Tangazo la Bwana Wetangula lilikinzana na uamuzi wa pale mbeleni ambapo muungano wa Azimio ambao ulikuwa na idadi ya jumla ya vyama 26 ambavyo vilileta wabunge 171 dhidi ya Kenya Kwanza ambayo ilikuwa na viama 15 ambavyo viliweka Pamoja idadi ya wabunge 165 mwanzoni,hivyo kuupa muungano wa Azimio nafasi ya kuwa na wabunge wengi bungeni.
Wakati ambapo Spika Wetangula alikuwa akitoa tangazo hilo alifafanua kuwa wanachama kumi na wanne(14) kutoka muungano wa Azimio walikuwa wameandikia afisi ya msajili wa vyama Bi Ann Nderitu wakiomba kujiondoa katikaa muungano wa azimio vikiwemo vyama vyao vinne.
Vyama vinne villivyojiunga na muungano wa Kenya kwanza kutoka azimio ni UDM, MDG, MCC na chama cha PAA ambapo jumla ya wanachama 14 waligura na kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza.
Kutokana na hili wengi watajiuliza itakuwa vipi ikikusudiwa kuwa katika uongozi wa kamati mbalimbali bungeni zinashikiliwa na viongozi wa mrengo wa kenya Kwanza akiwemo kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichungwa, mwenyekiti wa kamati ya bajeti miongoni mwa kamati nyingine muhimu kama ulinzi, afya, elimu na kilimo ambapo maauzi mengi yalishafanywa na kuamuliwa.
Kulingana na usemi wa mbunge wa Eldas Adan Keynan, alitaja uamuzi wa Mahakama kama uamuzi uliotolewa kwa kuchelewa akisema kuwa miungano ilisambaratika punde tu baada ya uchaguzi kukamilika.
Usemi kama huo ulitolewa na mwakilishi wa kike wa Kaunti ya Laikipia Jane Kagiri aliyedai kuwa kitakachosubiriwa ni kuona kama bunge litaheshimu uamuzi wa mahakama au la kauli hio ilisisitizwa na Mbunge wa Kirinyaga Njeri Maina.
David Ochieng Mbunge wa Ugenya alisema kuwa korti ilikuwa ikiacha bunge la taifa likiendesha shughuli zake pasi kuingiliwa hivyo basi uamuzi huo hadhani kama utakuwa na athari zozote ikizingatiwa kuwa watu na vyama walishapiga hatua nyingine ikiwemo kuteuliwa kwa mawaziri kutoka mrengo wa azimio.
Kikubwa kinachosubiriwa ni kuona iwapo bunge litatii uamuzi wa mahakama au litakataa rufaa kusitisha uamuzi huo vikao vitakaporejelewa hapo kesho.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!