Wakili ndegwa Njiru amesema kuwa atapinga uamuzi wa rais William Ruto kuwapa vitambulisho bila masharti wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Katika ukurasa wake wa X wakili huyo alikosoa amri ya rais akisema kuwa haifai na atafika mahakamani kupinga uamuzi huo.

''Wakenya wenzangu nitajitolea kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya rais ya kuondoa masharti ya kuwapa vitambulisho vya kitaifa wakazi wa mipakani bwana rais hautaharbu nchi tukiona wewe ni rais wa muhula mmoja na ni lazima utaenda nyumbani''wakili Njeru alieleza.

Matamshi hayo ya bwana Njiru yalishutumiwa vikali na wananchi waliomtaka kuomba msamaha kwa kuidunisha taaluma yake na nafasi yake kama wakili taajika.

"Anazungumza pasi kuyapima maneno yake..Wakili mzima kwenda mahakamani kueleza koti kuwa wakenya wengine wanastahili kutengwa ni mahakama gani itasikiliza madai yako ambayo ni kinyume cha katiba?'' Mohamed alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Akizungumza siku ya Alhamisi katika Kaunti ya Garissa aliweza kuwarai wananchi kutowasikiliza viongozi ambao wana nia na lengo la kuwagawanya na kuwapotosha wakenya kuhusu miiradi ya serikali akiwaeleza kuwa serikali ina mipango ya manufaa na ya kuwasaidia wananchi kujiendeleza kimaisha bali si kuwanyanyasa alizungumza akiwataka kuwa mstari wa mbele kuchanja mifugo wao.

Rais Ruto kwa sikuchace zilizopita amekabiliwa na mawimbi makali ya siasa kutoka kwa vijana mitandaoni pamoja na viongozi kutoka upinzani ambao wamekuwa wakimkashifu kwa kukaza uchumi na kuwatoza raia ushuru wa juu.  Aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua pamoja na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka wameonekana kuwa mbioni kumkata mizizi kwa kupinga ajenda za serkali.

Hali hii inapoendelea rais alitoa wito wa viongozi kutuliza joto la siasa na kampeni za mapema nchini na badala yake wajitolee na watumie nafasi hii kuelezea wananchi kuhusu umoja na mshikamano wa taifa pamoja na uzalendo kwa manufaa ya ustawi wa nchi.