
Wakili Donald Kipkorir asema hataki watu wamjumuishe katika makundi ya whatssap za matanga kwa kizingizio kuwa hakusaidiwa wakati mama yake alikuwa mgonjwa.
Kipkorir alisema kuwa anakumbuka vyema enzi ambazo mama yake alikuwa mjonjwa wa saratani hamna mtu alijitokeza kusimama naye katika kipindi hicho kigumu akikariri kuwa si haki watu washinde wakimjumuisha kwenye makundi ya matanga kwa mtandao wa whatssap.
Katika chapisho ambalo alichapisha katika mtandao wakae wa Whatssap siku ya Alhamisi 6,2025 bwana Kipkorir alisema hivi'' Kwa marafiki zangu na maadui wakati mama yangu alikuwa mgonjwa akiugua maradhi ya saratani kwa muda mrefu wengi wa marafiki zangu hawakuwahi kunitafuta kwa hivyo nashangaa mbona wao wakiwapoteza wapendwa wao wanataka mimi niwe kwa makundi yao.''
Wakili aliongezea akisema kuwa kwa sasa haoni haja ya kuwa na marafiki baada ya kupitia katika hali ngumu kama hiyo ''katika umri wangu kwa sasa sihitaji marafiki kwa vyovyote vile kama hukuwahi nitafuta enzi ambazo nilikuwa namuuguza mama yangu akiwa ngonjwa kwa sasa haina haja.''Donald alisema
Mamake wakili bi Karatina aliaga dunia mnamo mwaka wa 2023 Mei, 5 baada ya kupambana na maradhi sugu ya saratani bwana Kipkorir alipambana na ninake kwa kumtafutia tiba katika hospitali mbalimbali hadi kwenda nchi ya India ili aokoe maisha ya mzazi wake ila juhudi hizo ziliambulia patupu na mama yake akaikata roho mwishowe.
Bwana Kipkorir alitangaza mauko ya mamake kwa kusema kuwa ''mama kwa hakika umekuwa shujaa katika maisha yangu umepigana vita vikali tena vigumu nenda salama ukakae katika himaya ya Abrahamu mama pumzika salama''.Wakili aliandika kuashiria huo ndio ulikuwa mwisho wa kuwaka kwa mshuma wa maisha ya mamake duniani.
Kuna baadhi ya wakenya waliyachululia maandishi ya Kipkorir kwa mitazamo miwili tofauti kuna wale waliomuunga mkono kwa kusema kuwa waswahili walinadi kuwa nyege ni kunyegezana kwa hivyo kama zile enzi hukuwahi kumsaidia wakili wala kumpigia simu na ilhali ulikuwa rafiki yake wa karibu ni makosa kuuomba usaidizi wa michango kutoka kwake.
Kwa Upande mwingine wengine walijitokeza na kumkashifu kwa kutoa usemi ambao unaashiria bezo na madharau katika maisha ya wengine wakisema kuwa mtu hasitahili kulipiza kisasi badala yake atende wema na aende zake kuashiria kuwa anasitahili kukubali kuwekwa kwenye makundi ya whatssap na asaidie watu akirejelea usemi kuwa yaliopita si ndwele tugange yajayo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!