caption

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Januari 7.

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moj jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Kakamega, na Vihiga.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kilimani zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Eneo la soko ya Khwisero katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Kima katika kaunti ya Vihiga pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.