
Gavana wa Bomet Hillary Barchok alikamatwa na maafisa kutoka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC mapema leo asubuhi.
Gavana alikamatwa kwa tuhuma za ufujaji wa pesa za umma shilingi milioni 373 ambapo ana kesi ya kujibu kuhusu matumizi mabaya ya pesa za umma na vilevile anachunguzwa kwa kupatikana na stempu zaidi ya 100 pamoja na kununua vifaa 12 vyenye thamani ya shilingi 373 vya kujenga barabara.
Gavana Hillary Barchok ambaye alichaguliwa na wananchi kuongoza gatuzi hilo chini ya utawala wake amekuwa akipokea shutuma na lawama kutoka kwa viongozi pinzani pamoja na wananchi kwa kukosa kutimiza ahadi alizoahidi wananchi na badala yake amekuwa akiendeleza ufisadi badala ya miradi ya kujenga kaunti.
Kutokana na lalama hizo kutoka kwa wananchi pamoja na viongozi akiwemo Seneta wa kaunti hiyo Hillary Sigei wamekuwa wakimkashifu gavana kwa madai ya ufisadi na kuwa na maslahi ya binafsi huku akikosa kufanya maendeleo yanayohitajika.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC ilimkamata kwa madai ya ufisadi na vilevile simu za wafanyakazi wake ofisini zilichukuliwa kwa minajili ya kusaidia katika uchunguzi . Gavana Barchok alipelekwa katika kituo cha polisi cha Nakuru ambapo alihitajika kurekodi taarifa katika makao makuu ya tume hiyo.Tume ya EACC ina mamlaka kikatiba kukuchunguza na kuhakikisha kuwa mali ya umma inalindwa ipasavyo bali haifujwi na viongozi ambao wako madarakani.
Kulingana na mgao wa serikali ya kitaifa kwa magatuzi mwaka huu ilitoa takribani shilingi bilioni 354.59 kwa ajili ya serikali za magatuzi mgao huo ambao ni kiasi sawa na shilingi milioni 700 kwa kila gatuzi kutoka kwa serikali ya kitaifa,serikali hizi zikiongezea matozo ya ukusanyaji ushuru katika viwango vya kaunti gatuzi linastahili kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana kwa wingi.
Serikali za ugatuzi zina kazi anuwai ambazo zinastahili kuwa zinatekeleza kama ujenzi wa masoko,afya,baaadhi ya barabara,kilimo,maji,michezo na biashara wananchi waligatuliwa majukumu haya kutoka kwa serikali kuu ili ndio kuwe na uwazi na wepesi wa kutekeleza haya yote kwa hivyo ikiwa Gavana hatekelezi miradi yoyote kwa wananchi wake hiyo basi ni dhuluma na utumizi mbaya wa afisi na raslimali ya umma.
Magavana wote wanastahili kufahamu kuwa rekodi yao ya maendeleo ndio itawapa fursa ya uongozi wa awamu ya pili kwa kuzingatia tu iwapo walitimiza kile ambacho waliahidi wapiga kura bila hilo watakuwa na mchongoma wa kushuka .
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!