Hatimaye serikali imetoa mgao wa shilingi bilioni 3.32 za vyuo vikuu kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wa mwaka wa 2024 na 2025.

Katika taarifa yake waziri wa elimu Julius Ogamba alitangaza kutolewa kwa fedha hizo kupitia kwa bodi ya HELB alitangaza akisema kuwa bodi itapokea fedha ambapo itawagawia wanafunzi kwanzia kiwango cha shilingi 40,000 hadi 60,000 kwa kila mwanafunzi.

Serikali ilitoa jumla ya shilingi bilioni 3.32 mnamo Januari 31,2025 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili 2024/2025 ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wananufaika na kutumia hela hizo kukimu mahitaji yao ya kimsingi wanapoendeleza masomo yao.

Waziri Ogamba alikariri kuwa awamu hii ya utoaji wa hela hizo ilikuwa imeafikiwa Julai mwaka jana 2024 katika mkutadha ambao ulikuwa umeratibiwa katika bajeti ya mwaka jana na huu ili kuhakikisha kuwa mikakati ya usambazaji wa fedha kwa bodi husika inaafikiwa.

Mpango huu unajiri baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi walipoandamana wakilalamikia na wakikashifu bodi hiyo ya usimamizi na inayowapa wanafunzi mikopo kwa kuchelewa kutoa fedha hizo kwa wakati wakisema kuwa wamesubiri kwa muda kupewa mikopo ila bodi husika imesalia kimya na wakawa hawana budi ila kuandamana kushinikiza bodi kuwajibika ipasavyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Bodi inayosimamamia ugavi wa fedha kwa wanafunzi kupitia kwa kiongozi wao akijibu madai na tetesi za wanafunzi hao ilikubali kuwepo kuchelewesha kutoa hela hizo ikikiri kuwa hiyo ilitokana na kesi iliyokuwa imewasilishwa katika mahakama kuu kupinga mfumo mpya wa kutoa mikopo hiyo kwa wanafunzi.

''Kucheleweshwa kwa mikopo kunatokana na amri ya mahakama iliyozuia mfumo mpya wa kuwapa hela wanafunzi jambo ambalo lilisababisha bodi kusitisha kutoa mikopo hiyo kwa muda msimamizi mkuu wa HELB bwana King'ori Ndegwa alieleza.

''Kutokana na maamuzi ya mahakama imeilazimu bodi kusalia kimya tukisubiri kubatilishwa kwa maaamuzi ya mahakama yaliyoutaja mfumo mpya kinyume cha sheria lakini itatulazimu kurejelea mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu na nne'' .