Ni siku ya pili Kiongozi wa taifa akiwa Kaunti ya Mandera kwa ziara ambayo imeratibiwa kuelezea sera na miradi ya serikali eneo hilo la kasikazini mashariki ya Kenya.

Ruto alikariri waziwazi akisema kuwa taifa linakosa kusonga mbele kimaendeleo kwa sababu ya kuwa na viongozi ambao hawahubiri injili ya umoja na maendeleo bali wanajikita katika siasa za uongozi na vyeo.

Ruto alidai kuwa Kenya ingekuwa imepiga hatua kubwa kama viongozi wangekuwa na nia moja ya kuunganisha wakenya naRuto alidai kuwa Kenya ingekuwa imepiga hatua kubwa kama viongozi wangekuwa na nia moja ya kuunganisha wakenya nakuwapa mwelekeo mzuri ili kustaawisha uchumi na maendeleo kwa jumla.Rais alidokeza kuwa wakati wa kuzungumzia masuala ya uchaguzi u mbali na kwa wakati wa sasa viongozi wanastahili kuwafanyia kazi wananchi.

Akizungumzia kwa upana suala la uchaguzi mkuu wa 2027 rais alidokeza kuwa wale ambao wanazungumzia masuala na uongozi rais alisema kuwa ni mapema kuzungumzia uchaguzi ujao ila akawaeleza kuwa hata uchaguzi huo iwapo utawadia hatishiki kwa maneno ambayo wapinzani wake wamekuwa wakitema dhidi yake na utawala wake kwa jumla.

Rais alisisitiza akiwajibu kwa bezo kuwa yeye alikuwa mbunge kwa miaka kumi na mitano,akawa naibu wa rais kwa miaka kumi kwa sasa yeye ni rais kwa hivyo haoni haja wala hana wasiwasi wowote kutoka kwa wakosoaji wake wanaosema kuwa yeye ni rais wa muhula mmoja akisema kuwa wale wote wanaowazia hilo jambo wafahamu hio ni ndoto.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

''mimi nimekuwa mbunge kwa miaka kumi na mitano nikawa naibu wa rais kwa miaka kumi halafu mimi ni rais mtu anasema kuwa mimi nitakuwa rais wa muhula mmoja na ilihali anayesema hivyo hajawahi kuwa rais'' Daktari William Ruto alisema.

Rais alisisitiza kuwa ikifika mwaka wa 2027 atajitosa kinyang'anyironi kupambana na wanasiasa wengine akisema kuwa sasa jukumu lake kuu ni kujenga barabara,kuhakikisha kuwa watu wanapata nguvu za umeme, watu wanapata maji na kuboresha maisha ya wananchi kwa kupanga na kuhakikisha kuwa miradi yote ya serikali inatimizwa na inawafikia wananchi wote kote nchini pasi kubaguliwa .

Hapo jana rais aliweza kufutilia mbali vikwazo ambavyo vimekuwa vikiwazuia wakaazi wa eneo hilo la kasikazini mashariki ya Kenya akisema kuwa kama wakenya wengine wana haki sawa ya kupata vitambulisho bila kuulizwa maswali .