Mshambuliaji wa Colombia, Jhon Duran sasa atalazimika kusafiri kwa mwendo mrefu kila siku kwa zaidi ya kilomita 500 ili kuhudhuria mazoezi na klabu yake mpya ya Al-Nassr.

Uamuzi wake wa kuishi nje ya Saudi Arabia unachochewa na mkanganyiko sababu ni kwamba hana imani iwapo ataruhusiwa kuishi na mpenzi wake.

Chini ya sheria ya Kiislamu, wapenzi ambao hawajaowana rasmi hawakubaliwi kuishi pamoja kama mke na bwana na wamiliki binafsi wa nyumba mara nyingi hudai uthibitisho wa ndoa kabla ya kukubali kukodisha nyumba zao

Licha ya kuwa na tofauti, raia huyo wa Colombia ameripotiwa kuamua kukaa katika jimbo jirani la Bahrain na mpenzi wake, ambapo atasafiri kwenda mazoezini kila siku.

Safari ya ndege kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bahrain kuelekea mji mkuu Riyadh inachukua muda wa saa moja na dakika 20. Hili litamulazimu Durani kuwa na safari nyingi sana kila wiki.

Jhon Duran, mshambuliaji huyo sio mchezaji wa kwanza kuishi inje ya Saud Arabia bali kulikuweko na baadhi ya waliowahi kufanya maamuzi kama hayo.

Katika siku za nyuma Steven Gerrard, ambaye wiki hii aliondoka Al-Ettifaq kama meneja, na Jordan Henderson wote walichagua kuishi nje ya Saudi Arabia.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Uwanja wa mafunzo wa Al-Nassr uko nje kidogo ya Riyadh na zaidi ya maili 300 kutoka Bahrain.

Duran alifanya mabadiliko kutoka Villa Park kwenda Saudi Arabia baada ya kukosa muda wa kucheza kama mwanzo katika kikosi.

Uhamisho wake ulichangia ada ya pili ya uhamisho ambayo Villa wamewahi kupokea baada ya winga Jack Grealish kuhamia Manchester City kwa ada iliyoripotiwa ya pauni milioni 100 (dola milioni 124.05) mnamo 2021.

Duran alijiunga na Villa kutoka Chicago Fire kwa £ 18 milioni mnamo Januari 2023, akifunga mabao 20 katika mechi 78, lakini akicheza mechi saba tu za ligi ya uingereza