
Muigizaji mashuhuri wa Kenya Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ameingia kwenye maombolezo.
Muigizaji huyo mahiri yuko katika hali ya huzuni baada ya kumpoteza nyanya yake kipenzi.
Alitangaza habari hizo za kusikitisha kupitia akaunti yake ya Instagram siku ya Jumatano, akifichua jinsi alivyoumia sana moyoni.
"Shushu wangu mpendwa!" Kate aliandika kwenye Instastori zake na kuambatanisha taarifa yake na emoji ya moyo uliovunjika na uso wa huzuni.
Mama huyo wa watoto wawili pia alichapisha picha ya kumbukumbu yake na marehemu nyanya yake.
Alieleza jinsi alivyoumia moyoni na kumsihi mwanamke huyo aliyempenda sana arudi.
“Hii inauma sana. Shushu tafadhali rudi,” aliandika.
Kundi la mashabiki na wafuasi wake walimiminika chini ya chapisho lake la huzuni ili kumfariji, na kumtakia nguvu anapoomboleza.
Maureen Kunga: Praying for you my dear. Poleni san.
Luciah Njoki: The Lord is close to the brokenhearted.
Mutahi Kuria: May God comfort you and your loved ones.
Jackie Matubia: Woi pole may she rest in peace.
Kavinya Rose: Pole sana Cate. May Shosh find peace in her rest. My condolences to you and family mama.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!