MCHUNGAJI maarufu kutoka nchini Tanzania, Daniel Mgogo ametoa ushauri kwa wanaume wanaotaka kugharamia ada za elimu za wapenzi wao.
Katika moja ya mahubiri yake, Mgogo alisema kwamba wanaume wengi huhadaiwa kuwasomesha wachumba wao hata kabla ya ndoa na baadae kuishia kujuta baada ya wapenzi hao kutimkia kwa wanaume wengine katika ndoa.
Mgogo aliwasiositizia wanaume kwamba mchumba hasomeshwi, lakini mke akitaka kusomeshwa bila shaka msomeshe.
Kwa mujibu wa mchungaji Mgogo, wewe kama mwanaume na uko na mpenzi hujamuoa na anataka umsomeshe, basi mpeleke katika shule ya kutoa mafunzo ya kidini na akishafuzu unamtoa huko na kumuoa rasmi.
“Somesha mke, mchumba akisema anataka kusoma mpeleke Bible School. “Mwambie ukitaka shule ya Biblia nakusomesha mpaka digrii kwa sababu hata nisipokuoa utaenda kumtumikia Mungu,” Mgogo alihubiri.
“Wewe unataka mimi nikusomeshe ukawe mwalimu halafu baadae unageuka na kusema ‘aliyekuambia mimi nataka kusoma ni nani?’ wewe soma Bible School kama unataka nikusomeshe,” Alisema.
Mchungaji huyo alisema kwamba mwanamke yeyote anayetaka kusoma basi anafaa kuwajibisha wazazi wake kugharamia ada ya elimu na wala si mchumba mwenye hajafunga ndoa naye rasmi.
“Lakini kama unataka kuenda chuo kikuu, baba yako akauze viwanja na mashamba akakusomeshe. Ukitaka nikusomeshe mimi basi tufunge ndoa hapa nikuweke ndani halafu utokee ndani kwenda kusoma huko nikijua wewe ni mke wangu. Nasomeshaje mchumba,” alisema.
Mchungaji huyo alisema kwamba wanawake wengi wanaposomeshwa na mwanamume ambaye hawajaoana rasmi hufika chuoni na kubadili fikira kuhusu penzi na mwanamume huyo.
“Unafika kule ukiwa mwaka wa mwisho unakutana na mwanamume mwingine unabadili mawazo na unakuja kuniambia ‘ooh samahani mimi kwanzia leo nimefikiria nikaona wewe hatuendani’… ukimuuliza kuhusu hela zote ulizomlipia anakujibu ‘ahsante kwea ukarimu’…” alisema.
Mchungaji huyo alisema wanaume wengi baada ya kuambiwa kauli hii hushindwa kujizuia hisia zao za hasira na wengine hata hufikiria kutafuta kamba na kujitoa uhao.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!