Taifa la Marekani kupitia rais wake Donald Trump sasa linatishia kupiga breki misaada yote inayotoka kwake kuingia nchi ya Afrika Kusini.

Rais Trump akizungumzia hili aliandika kwenywe mtandao wake wa kijamii wa  X akilitaja taifa la Afrika kusini kama linalokiuka haki za kibinadamu.

Amesema kwamba hili limetokea kwa muda mrefu hasa swala la kunyang'a watu wengine ardhi, ila vyombo vya Habari vya ene hilo vimepuzilia mbali kuangazia swala hilo.

"Afrika Kusini inanyang'anya ardhi na kuwachukulia watu wa tabaka fulani vibaya sana. Ni hali mbaya kwamba Vyombo vya Habari vya upande huo havitaki sana kulizungumuzia kama ilivyoelezwa." Trump alichapisha.

Trump pia aliandika kuwa Serikali ya Marekani haitakaa kimiya ila itafanya jambo. Amesema kwamba yeye kama rais atasimamisha misaada yote ya kutoka Marekani kuingia katika Taifa hilo la Afrika.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"[Ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu, Kimusingi, linafanyika kwa wote kuona. Marekani haitakaa kimia kwa ajili ya hili, tutachukua hatua.
Pia, nitasitisha ufadhili wote wa baadaye kwa Afrika Kusini hadi uchunguzi kamili wa hali hii utakapokamilika" Rais wa Marekani alikamilisha maandishi yake.

Siku moja tu baada ya rais Donald Trump kuandika ujumbe huo serikali ya Afrika kusini imeonekana kumujibu moja kwa moja.

Rais Cyril Ramaphosa ametetea sheria hio mpya iliyopitishwa katika taifa la Afrika kusini akiitaja kuwa haijakiuka haki ya mtu yeyote. 

Amesisitiza kwamba Afrika Kusini ni Taifa la Kidemokrasia na nchi zingine kama Marekani wao pia wana sheria zao ambazo zinazunguka maswala ya ardhi.

"Afrika Kusini ni taifa la demokrasia ya kikatiba ambayo imejikita sana katika utawala wa sheria, haki na usawa.Serikali ya Afrika Kusini haijachukua ardhi yoyote.

Sheria ya Unyang'anyi iliyopitishwa hivi karibuni sio chombo cha kutaifisha, lakini mchakato wa kisheria uliopewa mamlaka kikatiba ambao unahakikisha upatikanaji wa ardhi kwa njia ya usawa na ya haki kama inavyoongozwa na katiba.

Afrika Kusini, kama Marekani na nchi nyingine, daima imekuwa na sheria za matumizi ya ardhi ambazo zinasawazisha haja ya matumizi ya umma ya ardhi na ulinzi wa haki za wamiliki wa mali." Ikulu ya Rais iliandika kwenye mtandao wa X.

Serikali ya Afrika kusini inaeleza kuwa ina imani kwamba swala hilo litajadiliwa baina ya serikali zote mbili na watafikia suluhisho.

"Tunatarajia kushirikiana na utawala wa Trump juu ya sera yetu ya mageuzi ya ardhi na masuala ya maslahi ya nchi mbili. Tuna uhakika kwamba kati ya ushirikiano huo, tutaweke uwazi bora na wa kawaida juu ya mambo haya." maandishi yaliendelea.

Ikulu ya rais Ramaphosa pia iliweka wazi kwamba hakuna msaada wanaopata kutoka katika serikali ya Marekani zaidi ya asilimila 17% ya dawa zinazosaidia kupigana na makali ya virusi vya UKIMWI.