KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 4.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kirinyaga, Tharaka Nithi, na Vihiga.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kahawa West, Kamae Road na Mathare zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mukangu na Gatina katika kaunti ya Kirinyaga pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Nkondi na Giekuri katika kaunti ya Tharaka Nithi yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Sehemu za eneo la Luanda katika kaunti ya Vihiga pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!