DEM wa Facebook kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu uhusiano wake na Oga Obinna unaoonekana kuwa baridi katika siku za hivi karibuni.

Wawili hao walikuwa gumzo la mitandaoni mwaka jana, shukrani kwa mlahaka wao mwema katika kipindi walichokuwa wakichambua matukio ya wiki kwenye channeli ya Obinna.

Hata hivyo, baadae walitania kutengana Dem wa FB akidai kwamba alikuwa amechukua mapumziko kutoka kwa shoo hiyo na Obinna lakini baadae tena wakaonekana pamoja kwenye kipindi hicho kinachopeperushwa kwenye mtandao wa YouTube.

Haikupita muda kabla ya kipindi hicho kutoendelea tena, jambo ambalo limefanya baadhi ya mashabiki wao kuhoji hali ya uhusiano wao, haswa mwaka huu ambapo hawajaonekana pamoja kwenye kipindi.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo na Mungai Eve, Dem wa Facebook alikwepa swali hilo akisema kwamba kwa sasa yeye ana malengo ya kumiliki gari aina ya Harrier ifikapo mwisho wa mwaka huu.

“Wewe nikome jamani, mimi bado ni mtoto. Sasa hivi naangalia my bright future, sina muda wa ndoa, sina muda wa mapenzi,’ Dem wa Facebook alijibu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo, Eve alikuwa wa haraka kumrekebisha akisema kwamba yeye hakuwa anauliza kuhusu mapenzi bali uhusiano wao kikazi, akisema kwamba alikuwa anafikiria wawili hao hawachumbiani.

Dem wa Facebook aliendelea kujieleza akisema;

“Mimi bado ni mdogo, ninataka kumiliki Harrier ifikapo Desemba. Nisiponunua Harrier huu mwaka jamani nitawaweka nyinyi wote kwa kundi la WhatsApp kunichangia. Sina muda na mahusiano ya kimapenzi, siwezi fukuzia vitu viwili kwa wakati mmoja. Mapenzi kwangu yatakuja baadae sababu mimi huchukulia hilo kama chaguo mbadala.”

Kuhusu jinsi watu walikuwa wanaona yeye na Obinna wanapendeza pamoja, Dem wa Facebook alisema;

“Ona, watu wanatupenda na hao ni watu. Hamwezi kujua kuhusu sisi na Mungu. Watu wanatupenda ndio lakini sisi wenyewe achana nasi. Muda ndio utasema ukweli, mimi bado ni mdogo.”

Mrembo huyo alisema kwamba kwa sasa lengo lake kuu ni kujitajirisha na kusisitiza kwamba hata hujawahi fikiria wala kujua ni nani atakayemuoa.

“Mimi hata kusema ukweli sijui nitaolewa na nani. Kwa sasa mimi nataka kujinunulia tu gari langu la Harrier sitaki kuzawadiwa. Nataka kupata ile hisia ya kujinunulia.”