MTENGENEZAJI maudhui na mchekeshaji Dem wa Facebook ametoa msimamo wake kuhusu kuolewa na mwanamume ambaye tayari ako na mtoto au watoto.

Akizungumza kwenye podikasti ya Hey Girl na Eve Mungai, Dem wa Facebook aliulizwa ikiwa yeye anaweza kubali kuolewa na jamaa ambaye tayari ana mtoto huko nje.

Mrembo huyo alikiri kwamba kwake haoni ugumu kukubali ndoa hiyo, akijitetea kwamba siku hizi wanaume wengi wana watoto kabla ya ndoa.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba anaweza tu kubali kuolewa na mwanamume mradi asiwe na watoto zaidi ya mmoja.

“Kusema ukweli Kenya sasa hivi 99% ya wanaume wako na watoto huko nje. Unapata wengine hata hawakuambii, ni wachache sana wanasema ukweli,” alisema.

“Watu wengi huwa wanasema hawajawahi ona mechi inaanza 1-0 lakini siku hizi inabidic tu ianze juu kupata mwanamume hana mtoto ni ngumu sana.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mrembo huyo alitoa kikwazo kwamba kando na kumkubali mwanamume mwenye mtoto mmoja tu, lakini pia mwanamume huyo asiwe ana ukaribu na babymama wake.

“Mtoto mmoja tu ikienda sana bora babymama aikuwe na drama. Kwa sababu watoto ni Baraka. Mimi nikipata mwanamume mwenye ako na mtoto mmoja na huyo mtoto akubali kuja kuishi na mimi ni sawa.”

“Mimi naweza ishi na mtoto wa mpenzi wangu. Juu siwezi kubali kufurahia maisha mazuri kwa hisani ya mpenzi wangu na mtoto wake anateseka huko nje,” aliongeza.