Aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka amedokeza kuwa atahakikisha kuwa rais William Ruto anashitakiwa katika mahakama ya jinai ya Kimataifa ya ICC iliyoko nchini Uholanzi.
Katika ujumbe kwenye mtandao wake wa X siku ya Jumapili Februari 2,2025 Kalonzo alidai kuwa Ruto ameongoza utawala ambao unaunga mkono na kushabikia utekaji nyara na mauaji ya vijana wadogo nchini.
''Ruto ameongoza utawala ambao unafadhiliwa na ikulu dhidi ya kuwateka nyara na kuwaua vijana wadogo ambao wanapigania haki zao za kikatiba.Tutampeleka katika mahakama ya jinai ya kimataifa ICC ili ajibu mashitaka dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu wakenya wameungana wamesema Ruto aende nyumbani." Kalonzo alisema.
Mwaka wa 2016 mahakama ya kimataifa ya ICC ilifutilia mbali kesi ya Ruto kwa ukosefu wa ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashitaka.
Katika uamuzi, jaji mmoja alisema ni kinyume cha haki katika jambo ambapo shahidi anahitalifiwa katika kutoa ushahidi kwa sababu ya maslahi ya siasa.
Ruto alikanusha mashitaka kuhusu mauaji, kuwafurusha na kuwafungulia mashtaka watu wakati wa vurugu iliyofuatia uchaguzi wa 2007 ambapo takribani watu 1200 waliuawa.
Katika miezi ya hivi majuzi tangu maandamano ya kupinga serikali yaanze mwezi wa Juni na Julai mwaka jana kumekuwa na visa vya utekaji nyara na mauaji ya kiholela kwa wale ambao wanaoonekana kupinga serikali.
Mmoja wa mawaziri wa Ruto bwana Justin Muturi tayari amejitokeza waziwazi na kuilaumu serikali kwa suala la utekaji nyara baada ya mwanawe kutekwa nyara mwaka jana, katika hafla tofauti na vyombo vya habari waziri huyo alisisitiza kuwa serikali ni lazima iangazie hilo swala kwa mkazo na msisitizo mkubwa badala ya kujihusisha na masuala mengine ya kimataifa ya kuleta amani huko DRC Kongo.
''Mwanangu alitekwa nyara na akatoweka sikuwa na uhakika ikiwa alikuwa hai au la jambo hili lilinifanya mimi na mke wangu kuwa katika hali mbaya sana pamoja na familia kwa jumla wakati huo nilikuwa mshauri mkuu wa serikali na mwanachama wa baraza la usalama wa taifa licha ya kufanya upelelezi ilikuwa vigumu kumpata''.
''Kwa sasa ni takribani miezi sita imepita serikali haijawahi mshitaki wala kumutaka andikishe taarifa katika kituo chochote cha polisi wala kuelezea ni kwa nini walimteka nyara ''
Vyombo vya usalama vimesema kuwa sivyo vinavyohusika katika utekaji nyara rais naye amekariri kuwa angependa kuona utekaji nyara ukikomeshwa mara moja wakenya wanataka kujua ni nani huyu anateka watu nyara ,ni vijana wangapi wametekwa nyara na ni wangapi wameachiliwa'' Muturi alieleza.
Mtoto wa Muturi Leslie alitekwa nyara mwezi wa Juni 22,2024 katika kilele cha maandamano ya vijana wa GEN Z kote nchini hatimaye Leslie aliachiliwa Juni 23,2024 saa chache baada ya kukamatwa kwake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!