CROSSDRESSER maarufu kutoka Nigeria, Okuneye Idris Olarenwaju maarufu kama Bobrisky amezua mjadala mpya baada ya kukiri kwamba aliwahi kumpa mwanamke mimba wakiwa chuoni kabla ya kubadili jinsia kupitia msururu wa upasuaji.


Bobrisky alitoa ungamo hilo wakati wa kipindi cha moja kwa moja cha maswali na majibu na mashabiki wake kupitia Instagram.


Bobrisky alidai kwamba kabla ya tukio hilo na mrembo aliyemtaja kwa jina moja tu – Lamide, yeye bado alikuwa bikira na mrembo huyo ndiye alimvunja ubikira wake.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwanamume huyo anayejitambulisha kama mwanamke pia alidai kwamba Lamide huyo ndiye aliyemtongoza wakiwa chuoni kwenye bweni katika chuo cha Lagos.


“Kwa hiyo usiku ule tulikuwa tukisubiri nani atagusana kwanza, mimi nilikuwa nimeegemea ukuta, alikuwa akinikabili. Kwa sababu nilikuwa na haya, sikujua nianzie wapi, sikujua la kufanya. Alianza kunishikashika na hatimaye tukafanya hivyo, hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza na pekee nilikuwa na mwanamke,” alisema.


Bobrisky, ambaye alikuwa katika mwaka wake wa pili katika chuo kikuu wakati huo, alikumbuka maoni yake wakati Lamide alipomwangazia habari juu ya Siku ya Wapendanao.


"Haikuwa hadi miezi miwili au mitatu baadaye. Siku hiyo ilikuwa hata Siku ya wapendanao. Kwa hiyo alininunulia singlendi, chupi na takrima nilizohitaji shuleni. Sasa alikuwa kama 'Bob mimi ni mjamzito Na nilikuwa kama' mjamzito vipi? Ulifanyaje? Shangazi mimi ni mvulana mdogo sana, nimeingia tu 200 level. Tafadhali usiharibu maisha yangu’,” alisimulia.


Alikiri kwamba alimwomba Lamide kuzingatia "suluhisho" kwani hakuwa tayari kuwa baba wakati huo.


“Kisha nikamwambia tunahitaji kutafuta suluhu kwa sababu sikuwa tayari. Alijua mimi ni mwanamke kidogo lakini sio mwanamke huyu. Sijui labda alinipenda kwa sababu nilikuwa mwanamke, sikuweza kujua."


Hata hivyo, Lamide alikataa na baadaye kumripoti kwa kundi la wavulana, ambao walikabiliana naye kuhusu hali hiyo.


"Alisisitiza kwamba angezaa na akaanza kunitukana, akanitoa wa kike na mimi pia nikaanza kumtupia matusi," alisema.


Hii si mara ya kwanza kwa Bobrisky kuzua kauli za kuchanganya wafuasi wake.


Mwaka jana, alizua maoni kinzani alipodai kwamba ameanza kuona hedhi yake ya kila mwezi baada ya kukamilisha upasuaji wa kubadili jinsia kabisa.


Aliwahurumia wanawake ‘wenzake’ akisema kwamba hakuwa anajua hedhi huja na uchungu kiasi hicho lakini akasema kwamba alikuwa tayari kukabiliana na changamoto mpya ya kuwa mwanamke.