MILKA Moraa, mwanamke kutoka mtaa duni wa Mukuru kwa Njenga aliyeonekana kwenye video akidhalilishwa kanisani kwa Pasta Ng’ang’a wakati akimuomba msaada wa kodi ya nyumba amepata nafasi ya kuanza upya kimaisha, shukrani kwa umoja wa Wakenya.


Mwanamke huyo alikwenda katika kanisa la mchungaji huyo na kusimama akiomba msaada wa kodi ya nyumba kwani alikuwa amefungiwa nyumba kwa Zaidi ya wiki moja.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika video hiyo ambayo iliwatia huruma Wakenya wengi, mchungaji huyo wa Neno Evangelism alimfukuza akimwambia kwamba yeye si wa kutoa misaada na kumtaka aende kuishi kwa nyumba za bei nafuu zinazojengwa na serikali ya William Ruto.


"Mchungaji nimefungiwa nyumba wiki moja sasa," Milka alisema huku akitokwa na machozi.


“Enda polisi hapo. Polisi yako wapi? Sasa umefungiwa, umekuja kutafuta pesa. Hapa ni kwa maombi. Kama ni mambo ya maombi, sawa. Pesa, enda kwa cabinet. Enda kwa Sakaja,” Ng’ang’a alimlipua


“Si kuna nyumba zimejengwa zinaitwa affordable? Si uende ukae hizo za affordable? Ndio nasema shida ya nyumba usiniletee. Shida ya nyumba enda kwa serikali. Mimi ninashughulika na mambo ya kiroho. Mambo kuhusu pesa, usije hapa ukitarajia pesa,” Ng’ang’a aliongeza.


Wakenya waliojawa na mioyo ya huruma waliungana kwe nye mitandao ya kijamii wakiongozwa na afisa wa polisi Sammy Ondimu Ngare ambapo kufikia wakati wa kuchapishwa kwa Habari hii, alikuwa amechangiwa Zaidi ya sh240k.


Katika nukuu iliyoambatanishwa na wadhifa huo, Ondimu alibainisha kuwa yeye mwenyewe hakuweza kuamini kwamba Wakenya wanaweza kujitolea kumsaidia mtu kwa njia kubwa na akasema kwamba, kweli, Milka (mwanamke aliyetajwa) alibarikiwa kweli.


“Hakuna kama Yehova. Milka amebarikiwa. Tumefika 240k sasa. Waendelee kuja. 100, 200, 500, 1k, 2k, 5k zako. 0705028977 Milka Tegisi. Nitamtembelea Mukuru Kwa Njenga. Nani ako tayari twende,” alishiriki.