DOREEN Moraa Moracha, shujaa wa kupigana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI anasherehekea miaka 20 tangu aanze kutumia dawa ya kufuzaba virusi hivyo, ARVs.


Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mrembo huyo alichapisha ujumbe huo akisema mwaka huu, alianza mwaka wake wa 20 katika safari ya kutumia dawa hizo na anashukuru Mungu Maisha yake yamekuwa katika mkondo salama kwa muda wote.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Moracha alisifia dawa za ARV kwa kuwapa watu wanaoishi na virusi vya HIV nafasi nyingine ya kuishi licha ya kwamba dunia bado haijapata tiba kamili ya virusi hivyo.


“Nilianza mwaka wangu wa 20 wa kutumia ARVs mwaka wa 2025. Bado hatuna tiba ya VVU, lakini ni lazima tupatie ARVs maua yake.Kwa ajili ya kuwaweka hai watu wanaoishi na VVU.”


“Kwa kukandamiza mgeni mdogo tunayemkaribisha, ili tusiweze kumwambukiza mtu yeyote VVU. Kwa kutupa nafasi ya kufanya jambo hili la maisha kama kila mtu mwingine. Kwa kutufanya tujue ukweli wa kuwa wakuu kuliko ukimwi kila siku,” Moracha alichapisha.


Historia ya Maisha ya mrembo huyo kutoka Kisii ni moja yenye wingi wa matumaini kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.


Kwa mujibu wa shirika la IAS kwenye tovuti yao, Moracha Alizaliwa na HIV, na aligundua hali yake alipokuwa na umri wa miaka 13 tu. Unyanyapaa na uchovu wa matibabu ulimfanya afanye siri na kuacha matibabu kwa miaka miwili.


"Nilipozaliwa, mama yangu hakujua yeye au mimi nilikuwa na HIV. Nilianza kuugua tangu mwezi wangu wa sita. Wazazi wangu na watu wa ukoo walidhani kwamba nilirogwa kwa sababu nilikuwa mgonjwa siku zote,” alihadithia katika simulizi la awali.


Ila baada ya kugundua hali yake, mwaka 2011 Moracha aliikubali hali yake na kuamua kuishi kwa njia chanya na virusi na mwaka 2015, aliamua kujitokeza kimasomaso kutoa hamasa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo lakini pia kuanza kupinga unyanyapaa wanaopitia waathirika.


Doreen sasa ni mshawishi wa mitandao ya kijamii aliyeko Nairobi, Kenya, na mwanzilishi wa chaneli ya YouTube ya I AM A BEAUTIFUL STORY. Anatumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kuwaonyesha watu wanaweza "kuishi maisha yao bora", hata wakiwa na virusi vya HIV. Pia amekuwa akifanya kazi na IAS - Jumuiya ya Kimataifa ya UKIMWI - kuunda Kituo cha Vijana, nafasi ya kidijitali kwa wafanya mabadiliko wachanga wanaoishi na kuathiriwa na VVU.