Utekaji nyara wenye utata na vifo vya kushangaza  vya watu wanne  kutoka maeneo ya Mlolongo vimeibua maswali mengi kuliko majibu nchini jambo hili likichochea mwanaharakati na Seneta wa Busia Okiya Omtatah kufika kortini kuishitaki serikali akitaka majibu kuhusu  vifo vyao.

Kisa hicho cha kushangaza kimeathiri taifa tangu  Desemba 17,2024 na kuchukua mkondo tofauti baaada ya watu wawili walioripotiwa kutoweka Justus Musyimi na Martin Mwau kupatikana wameuawa Alhamisi ya Januari 30,2025.Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X Alhamisi Usiku Omtatah alisikitikia  vifo  hivyo akitaka vyombo vya usalama kuwajibika ipasavyo.

''Ni masikitiko makubwa kupata habari za vifo vya Justus Musyimi na Martin Mwau wa kutoka Mlolongo waliotekwa nyara Desemba 17,2024, jioni nilikuwa na Duncan Kyalo kakake marehemu Justus Musyimi nikimfariji pamoja na jamii kwa jumla wakati huu mgumu ninasimama na wakenya wengine tukishiniki''Ni masikitiko makubwa kupata habari za vifo vya Justus Musyimi na Martin Mwau wa kutoka Mlolongo waliotekwa nyara  Desemba 17,2024, jioni nilikuwa na Duncan Kyalo kakake marehemu  Justus Musyimi nikimfariji  pamoja na jamii kwa jumla  wakati huu mgumu ninasimama na wakenya wengine tukishinikiza na kudai haki za hawa vijana ambao hawana hatia ambao wameaga kutokana na utekaji nyara.''omtatah aliandika'' .

Chapisho lake lilivutia umakini wa viongozi wa usalama wakiwemo mkuu wa polisi wa taifa na mkuu wa kitengo cha ujasusi  akisema kuwa hao ndio waweze kuwajibikia vifo hivi vya kinyama kwa binadamu(heinous crime againest humanity).''Taasisi za usalama ni lazima ziwajibike na zitoe majibu na kuelezea ni kwa nini vitendo hivi vinatendeka pasi kuwatambua watekelezaji la sivyo wakuu wa usalama wanastahili kujiuzulu na kutoka katika afisi za umma Omtatah alsema''.

Kwa sasa Omtatah analenga kuenda katika mahakama ya Milimani Ijumaa Januari 31,2025 kutaka majibu kutoka kwa serikali.Kesi hiyo inaazimia kuwaajibisha na kuuliza asasi husika za usalama kuhusu kutoweka kwa watu hawa na ikiwezekana wawajibishwe ipasavyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

''Kesho tutakuwa katika mahakama ya Milimani kushinikiza kupata majibu kutoka kwa  serikali kutokana na huu unyama na ukatili kuhusu binadamu tusimame pamoja kukataa visa vya utekaji nyara na vifo maliza utekaji nyara kenya Omtata aliandika katika ukurasa wake wa X hapo jana.''

Watu wanne kutoka Mlolongo Justus Mutumwa ,Martin Mwau,Karani Mwema na Steve Kavingo walitoweka mnamo Desemba 16,2024 miili ya Musyimi na Mwau ilipatikana siku ya Alhamisi wakati ambao mkuu wa polisi  Douglas Kanja na mkurugenzi mkuu wa kitengo cha ujasusi Mohammed Amin walipofika mbele ya Jaji Chacha Mwita  katika mahakama ya Milimani Nairobi kuelezea waliko wanne hao.

Akizungumza akiwa kizimbani mkuu huyo wa kitengo cha ujasusi alisema kuwa watu hao hawakuwa katika rumande hivyo ingekuwa vigumu kwa asasi za usalama kuwawasilisha jinsi katiba inavyosema, punde tu baada ya Amin kutamatisha kutoa ushahidi wake miili ya Musyimi na Mwau ilipatikana.

Vifo vya Musyimi na Mwau vimechochea hali ya sintofahamu nchini huku wengi wakikariri kuwa enzi za kutumia nguvu kupita kiasi zimerudi na mauaji ya kiholelaholela hali hii ikiendelea kupoteza imani ya usalama kwa wananchi,upande mwingine mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani na kulalamikia visa vya utekaji nyara ambavyo vinasababisha kukosekana kwa raia hao hata hivyo imani ya Wakenya inazidi kudorora kufuatia vyombo vya usalama kutotia bidii kutegua kitendawili hiki. Kwa sasa macho yote yanaelekea kwa mahakama kupiga msasa kubaini iwapo haki itapatikana kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.