MWANASOSHOLAITI Huddah Monroe ambaye mara nyingi hufanya shughuli zake kutoka nje ya nchi amefichua uzoefu wake kutangamana na wakenya wanaoishi nje ya nchi.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Huddah alidai kwamba Mkenya pekee unaweza kuamini kama rafiki wa kweli ni yule anayeishi humu nchini.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mremo huyo mjasiriamali katika fani ya bidhaa za urembo alisema kwamba Wakenya wanaoishi nje ya nchi ni pepo chafu ambao yeye hawezi kuwa na ukaribu nao.


Huddah alisema kuwa yeye akiwa nje ya nchi na akutane na Mkenya, anamkwepa kama ukoma kwa kile alisema kuwa kuwakaribisha ni saw ana kujitongea umbea usio na afya.


“Wakenya wa Diaspora mshindwe pepo chafu. Wakenya wa KENYA ndio watu pekee wa kweli unaweza fanya marafiki zako. Nje ya Kenya siwezi hata sema ‘hi’ kwa Mkenya. Nawapita mbio sana kwa sababu kusimama nao ni umbea wa ufala,” Huddah Monroe alisema.


Kauli ya Huddah inajiri siku chache baada ya madai kuibuka kwamba Wakenya wanaoishi USA wanawaripoti wenzao wasio na stakabadhi halali na kuwepo huko.


Hii ni baada ya rais mpya Donald Trump kutoa amri ya kukamatwa kwa raia wa Kigeni nchini Marekani wanaoishi kinyume cha sheria.


Katika siku chache zilizopita, baadhi ya Wakenya wanaoishi Marekani wamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii (Tiktok) wakidai kuwa ICE ilikuwa inalipa $750 (Sh96,900) kwa yeyote anayeripoti wahamiaji haramu kwa kufukuzwa, wanadai utekelezaji huo ulipuuzwa kuwa sio kweli.


Shirika hilo linalenga wahamiaji wowote kati ya wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 11 nchini humo bila hadhi ya kisheria, sio tu wale waliotambuliwa kama vipaumbele vya kufukuzwa kwa kuhukumiwa wahalifu au vitisho vingine vya usalama wa umma.