MSANII wa EMB Records, Bahati Kioko ametoa tamko la kejeli kwa wasanii wengine akisema kwamba kama walishindwa kutengeneza pesa wakati yeye na Willy Paul walikuwa hawapatani basi asahau kuwa Tajiri.
Bahati alikuwa anazungumza katika video moja akiwa na Willy Paul katika maandalizi ya mwisho kuelekea kuachiliwa kwa kolabo yao.
Bahati alidai kwamba kama kuna msanii yeyote aliyeshindwa kuchukua fursa ya bifu lake na Willy Paul kutengeneza pes abasi atakufa maskini kwani wawili hao tayari wamerekeisha urafiki wao.
Alijipiga kifua akisema kwamba yeye na Willy Paul ndio wasanii pekee wamekuwa wakishikilia tasnia ya burudani nchini kwa miaka 10, na kama hiyo haitoshi, ndio tena wameanza upya wakiwa marafiki.
“Unajua sasa hivi ndio tumeanza, ni enzi mpya na ujue bado sisi ndio tumekuwa tukishikilia kwa miaka 10 na ndio tunaanza tena. Hivyo kama kuna msanii hakutengeneza pesa huo wakati ajue sasa atakufa maskini maana sisi tumerudi,” Bahati alisema huku Willy Paul akimuunga mkono kwamba hii ni enzi ya kuwafuuza wasanii wa kigeni kutoka kilele cha chati za muziki humu nchini.
Alhamisi, wawili hao ambao wamekuwa wakihasimiana kwa miaka kadhaa walitangaza kuja Pamoja na kuachia kolabo mbili kwa mpigo.
Walitangaza kolabo hizo zingeshuka mapema Ijumaa asubuhi na upekuzi wa haraka, tayari kufikia muda wa kuchapishwa kwa ripoti hii walikuwa wameachia ngoma ya kwanza kwa jina ‘Paah’.
Ngoma nyingine ambayo wamefanya Pamoja na ambayo ingeshuka muda sawia inaitwa ‘Keki’.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!