Baraza la mitihani nchini KNEC limetoa mwongozo kwa wazazi,wanafunz na wakuu wa taasisi za elimu  jinsi ya kujisajili katika mfumo  wa  elimu wa KEPSEA na KILEA mtawalia.

Katika notisi iliyotolewa na afisa mkuu mtendaji wa KNEC David Njengere aliarifu wanafunzi pamoja na washikadau kuwa zoezi maalumu la kujifunza jinsi ya kujisajili litatamatika Februari 28,2025 baada ya kung'oa nang'a Januari 27,2025.

Kulingana na muongozo  wa KNEC taasisi au shule ambazo zina wanafunzi wa gredi ya sita watalazimika kuwasajili wanafunzi wao upya kufuata muongozo wa KNEC wa KPSEA kwa kitovu cha KNEC kimtandao(KNEC Registration Portal).Baraza hilo la mitihani limeelezea kwa upana kuwa wanafunzi watakaojiwasilisha kwa ajili ya kupigwamsasa ni lazima wawe wanatoka katika vyuo vinavyojulikana na wao pia wawe wanafahamika.

''Kuwasajili wanafunzi hewa kutavutia adhabu kali ikiwemo kufutilia mbali kwa shule hiyo jinsi KNEC inavyokariri katika notisi ilio na maelezo hayo,urekebishaji wa deta za wanafunzi lazima ufanyike wakati wa zoezi la usajili  ili kuhakikisha kuwa  maelezo ya mwanafunzi huyo yanakuwa sahihi  ili kupunguza makosa ya hijai, kusajili mwanafunzi kwa jina ambalo si lake, ambapo usajili huo wafaa uwe unalingana na majina yalio kwenye cheti chake cha kuzaliwa,jinsia,tarehe za kuzaliwa na uraia wao unanakiliwa ipasavyo KNEC  ilieleza.

Hata hivyo Baraza hilo la mitihani limesisitiza kuwa uhamishaji wa wanafunzi ni lazima utekelezwe ndani ya muda uliotengwa ambapo utafikia kikimo Februari 28,2025.''wanafunzi wa KEPSEA  ambao hawajajisajili katika gredi ya sita ni lazima wajisajili kwa mtambo wa gredi ya sita mwanzo(grade six Portal) ndio wapewe nambari ya udhibitisho .Wanafunzi ambao hawana nambari ya udhitibisho  hawatakubalika kujisajili kwa KPSEA.,kwani nambari hiyo itakuwa ni hitaji la lazima kufuatia kufaulu kudhibitisha nambari ya kujitambulisha, wakuu wa shule watapewa kibali cha kuwasajli wanafunzi wao''.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wakuu wa shule ni sharti wadhibitishe kwa mtambo wa shule(School portal ) kuwa mtaala wa shule  school based Assesment (SBA) wa gredi ya nne na tano uko katika mtambo huo'' portal'' na kila mwanafunzi amefanyiwa usajili wa sawasawa.

Kuhusu viwango maaalum  vya wanafunzi Baraza limeelezea vyema kuwa kwa wanafunzi ambao wanatarajiwa kujisajili kwa kiwango cha KILEA  watapewa muongozo  kutoka kwa walimu wao  baada ya walimu hao kudhibitisha kuwa wako taayari kupigwa msasa, hata hivyo wanafunzi ambao hawana uraia rasmi watalazimika kulipa  shilingi mia saba hamsini(750=) iili waweze kupigwa msasa wa kuwatathimini walipe  hela hizo kwa mtandao wa kielekrtroniki(E- Citizen).

''Kulingana na kifungu nambari 25,26 na 29 cha sheria   ya ulinzi wa deta ya 2019, wasimamizi wa shughuli hii wawafahamishe wazazi na walezi wa watoto kuwa habari kuhusu deta zao zitatumika tu kwa sababu ya mambo yanayofungamana na elimu wala si vinginevyo mwanafunzi atatia sahihi ya kudhibitisha uwajibikaji baada ya kukagua na kudhibitisha deta zake'' wizara ilieleza.