NAHODHA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars Michael Olunga ameonyesha furaha yake baada ya klabu yake ya Al Duhail ya nchini Qatar kumsajili aliyekuwa winga wa Chelsea, Hakim Ziyech.


Al Duhail ilitangaza usajili wa mchezaji huyo wa Morocco ambaye alikatisha mkataba wake na miamba wa Uturuki, Galatassary.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kutoa tangazo hilo, Olunga kupitia ukurasa wake wa X aliandika ujumbe wa kumkaribisha Ziyech kwenye klabu hiyo huku akimalizia kwa emoji ya tabasamu.


“Karibu Hakim,” Olunga aliandika.


Ziyech alitambulishwa Alhamisi jioni na klabu ya Ligi ya Qatar Stars baada ya kuondoka kwake kwa njia isiyo ya kawaida kutoka Galatasaray.


"Al-Duhail Sports Club ilifanikiwa kupata saini ya mchezaji wa kimataifa wa Morocco Hakim Ziyech," taarifa ya Al Duhail ilisema.


Winga huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 31 aliichezea timu ya taifa ya Uholanzi katika ngazi ya vijana na atacheza chini ya bosi wa zamani wa Paris Saint-Germain Christophe Galtier.


Hapo awali alijiunga na Galatasaray kwa mkopo kutoka Chelsea mnamo 2023 lakini alitofautiana na meneja Okan Buruk.


Mwezi uliopita, alisema hataki kuichezea klabu hiyo tena katika ungamo la kikweli lililozua mjadala mkubwa Zaidi kwenye ulimwengu wa soka duniani.


"Ukurasa Galatasaray umefungwa kwangu. Sitaki tena kucheza hapa. Ninaondoka Januari," alinukuliwa na jarida na spoti la GOAL.


"Sijawahi kuona kocha wa kiwango cha chini namna hii. Sijali sana [kama kujiunga na Galatasaray lilikuwa kosa]. Nataka kuachwa peke yangu, bila kujali kitakachotokea. Ninajuta kuja hapa."


Olunga ambaye miezi michache iliyopita aliweka rekodi kama mchezaji mwenye mabao mengi Zaidi katika historia ya klabu ya Al Duhail amekuwa katika klabu hiyo tangu 2021 na kushinda taji la 2023.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pia alishinda viatu viwili vya Dhahabu vya Ligi ya Qatari Stars.


Sasa ataungana na Ziyech mshindi wa Ligi ya Mabingwa akiwa na Chelsea. Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alikuwa sehemu ya timu ya Morocco iliyoshiriki Kombe la Dunia la 2022