Mnamo Jumatano Januari 29,2025 Sarah Wairimu alijiwasilisha katika mahakama kuu ya  Kibra mbele ya Jaji Diana Kavenza ambapo alikariri kuwa hana ufahamu wowote kuhusu kifo cha aliyekuwa bwana yake marehemu Tob Cohen mnamo mwaka wa 2019.

Wairimu alielezea mahakama ushahidi wake baada ya Hakimu Kavenza kutupilia ombi la afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma( DPP) Renson Ingonga lililoasilishwa na wakili Vincent Monda la kumtaka mshukiwa kufanyiwa vipimo vya akili kutupiliwa mbali na Jaji Kavenza.

Akitoa uamuzi huo jaji Kavenza alisema kuwa haikuwa na haja mshitakiwa kurudia vipimo kwa mara ya pili baada ya kufanyiwa vipimo vya awali

'Ombi la mwendesha mashitaka la kutaka mshukiwa afanyiwe vipimo vya akili kwa mara ya pili limekataliwa Hakimu Kavenza alisema'.

Mnamo Januari 24,2025 mkurugenzi na mwendeshaji wa mashitaka ya umma (DPP) Renson Ingonga kupitia kwa wakili wake Vincent Monda aliarifu korti kuwa Sarah Wairimu ni lazima angepata vipimo vya akili kabla ya kusikiliza ushahidi wake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

'Hii  mahakama haiwezi sema kuwa  Wairimu ni timamu ni lazima kuwe na ripoti hivyo basi tunairai hii mahakama kumwamuru mshukiwa afanyiwe vipimo vya akili hatimaye awasilishe ushahidi wake'wakili Vincent Monda alielezea mahakama.

Hata hivyo kupitia kwa mawakili wanaomwakilisha Bi Wairimu  wakiongozwa na wakili Conrad Maloba alipinga ombi hilo la mwendeshaji wa mashitaka akisema kuwa hakusema ikiwa alihitaji vipimo vingine mwanzoni.

'Hakuna haja ya mshukiwa au mshitakiwa kurudia vipimo vya akili wakili Maloba alisema'

Hakimu Kavenza aliamuru mshukiwa Bi  Wairimu arudi rumande ya wanawake ya  Lang'ata hadi Jumatatu Februari 3,2025 wakati ambapo mwedesha mashitaka atatuma ombi la kupinga kuachiliwa kwa mshitakiwa kwa dhamana wakati ambapo wakili wanaomtetea wanafanya juhudi kuhakikisha anapewa dhamana.

Sarah Wairimu alikamatwa alhamisi Januari 23, 2025 baada ya afisi ya mkurugenzi na mwendesha mashitaka ya umma(DPP) kusema kuwa ilikuwa na ushahidi wa kutosha unaonyesha kuwa Wairimu aliua mumewe Tob Cohen usiku wa Julai 19 na 20, 2019 katika mtaa mdogo wa Kabete jijini Nairobi.

Wairimu alikamatwa kwa mara ya kwanza 2019 baada ya mwili wa mumewe kupatikana kwa tangi katika mtaa wao wa Kitisuri,ambapo alishitakiwa kwa kosa la mauaji lakini baadaye kesi hiyo ilitupiliwa mbali.