KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Januari 30.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Narok, Isiolo, Kilifi, Kwale.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kasarani, Naivasha Road Kingara Road, Hatheru Road na Wanyee Road zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Narok katika kaunti ya Narok zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maeneo ya Merti, Bisan Biliqo, na Bulesa katika kaunti ya Isiolo yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa tisa alasiri.

Eneo la Rabai katika kaunti ya Kilifi litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi n moja jioni.

Sehemu z Diani Beach Road katika kaunti ya Kwale zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.