WALIOKUWA wasanii wa injili ambao sasa wanafanya vizuri katika fani ya miziki ya kidunia, Bahati Kioko na Willy Paul wametoa taarifa njema kwa mashabiki wao kuhusu ujio wa kazi zao za kikoa.
Kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, Willy Paul na Bahati walichapisha picha wakiigiza picha maarufu ya wanasoka Messi na Ronaldo wakicheza chess na kufichua kuwa wametoka jikoni tayari kuandaa kolabo zitakazoashuka kesho Ijumaa.
Pozee alifichua kwamba yeye na Bahati, ambaye tangu warekebishe urafiki wao Novemba mwaka jana wamekuwa wakirejeleana kama ‘kaka’ wanatarajiwa kutoa kolabo mbili kwa mfululizo kesho.
“Wafalme 2, Nyimbo 2, Shida Maradufu. Nyimbo Zote Mbili Zinadondoshwa Kesho Saa nne kamili Asubuhi. Waambie Wasanii Uliowapenda Washikilie Matoleo Yao Kwanza. Tunaiifanya kwa ajili ya Tasnia ya Muziki ya Kenya... Hebu Turudishe nuru yetu. Videos Kesho Ni Za Majuu Zote! @bahatikenya Huu Ndio Wakati Bro One Love,” Willy Paul alitamba.
Kwa upande wake, Bahati aliyaradidi maneno ya Willy Paul na kuwataka makada wake kuwa ange tayari kwa ajili ya mapokezi ya ngoma hizo.
Ukurasa mpya wa mlahaka wa wawili hao ulianza Novemba mwaka jana pale Pozee alivyoandika barua ya wazi kwa Bahati akimtaka samahani kwa mambo yote aliyowahi kufanya na kuzorotesha ukaribu wao.
Paul alimtaka Bahati kumsamehe kwa kile alijuta kwamba alikuwa akivuta majina na picha za familia ya Bahati kwenye mitandao ya kijamii na kueneza uhasama zaidi.
“Nikikumbuka mambo niliyojionea na kaka yangu, ninatambua kwamba mara kwa mara nimevuka mipaka. Ninashikilia sana dhana ya familia, haswa watoto. Matendo yangu hayakukusudiwa kamwe kusababisha madhara, lakini ninaelewa kwamba yalionekana hivyo, na ninaomba msamaha kwa Diana na watoto Kwa Upendo wa Kutokuelewana,” Willy Paul aliandika.
Bahati alimjibu akimwambia kwamba mambo ya dunia hayangewatenganisha huku akikumbuka jinsi walianza safari ya muziki pamoja miaka ayami nyuma.
“Ndugu Yangu @willy.paul.msafi ,Msamaha Umekubaliwa ? Tumetoka mbali, Sote tumepambana na changamoto nyingi na umasikini mkubwa katika Vitongoji duni vya Mathare ili kuwa hivi tulivyo leo na tunapojitahidi kuinuka na kuwa wakuu katika njia tumefanya makosa mengi lakini cha muhimu ni kurudi nyuma na kurekebisha pale tunapofikiri tulikosea kwani Mungu wetu ni Mungu wa Upendo na nafasi ya Pili. Zaidi ya yote hakuna kosa kubwa kuliko udugu tunaoshiriki,” Bahati alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!