Shirika la afya duniani (WHO) limeelezea hofu yake kwa taifa la marekani kujiondoa katika mradi wa ufadhili wa pesa katika programu ya kupambana na virusi  vya ukimwi katika mataifa  yaliyo na mapato ya wastani na ya chini kufuatia tangazo alilolitoa rais wa Marekani Donald Trump.

Kulingana na shirika hilo, mradi huu hutoa huduma za kuokoa maisha kwa zaidi ya watu milioni thelathini kote duniani.

Hata hivyo shirika hilo linakariri kuwa kujiondoa kwa taifa la Marekani katika ufadhili wake kunawaweka waathiriwa wa maradhi haya ya ukimwi katika hatri ya kifo na kusambazwa kwa wingi kwa maradhi haya.

katika taarifa yake nikinukuu "Kusimamisha ufadhili wa pesa katika programu ya maradhi ya Virusi vya Ukimwi  kunawatia waathiriwa wa ndwele hii katika mauti na kurudisha chini kila juhudi zilizopigwa za kukabiliana na kudhibiti kusambaa kwa maradhi haya na ikiwa ufadhili huu hautaendelea basi tutakuwa tumerudi nyuma katika enzi za miaka ya zamani ambapo watu walifariki kwa wingi kwa kukosa kinga hio miaka ya 1980 na 1990 kote duniani likiwemo taifa la marekani".

Shirika hilo limerai utawala wa Trump kutositisha ufadhili wake katika mataifa yanayoendelea kote duniani. "Tunaomba serikali ya marekani kutathimini na kuangazia msaada wake katika mataifa yanayokua,"

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Aidha, shirika hilo limekariri kuwa kujiondoa kwa ufadhili wa programu kutoka kwa taifa hili la Marekani ni kupiga hatua kadhaa nyuma pamoja na mfumo wa teknolojia  ya sayansi.

Taifa la Kenya ni mojawapo ya mataifa ambayo yameathirika kufuatia tangazo la Donald Trump  kuhusu kujiondoa kwake katika ufadhili wake.

Itakumbukwa wazi kuwa mnamo Januari 20,2025 siku ya kwanza ya rais Trump ofisini alitia sahihi sheria ya kusitisha ufadhili wa Amerika kwa mataifa mengine kwa siku tisini.

Baadhi ya misaada iliyositishwa ni dawa za kupunguza maradhi ya ukimwi, malaria na dawa za kifua kikuu kwa mataifa yote ambayo hupokea msaada huo.

Taarifa au memo iliyotumiwa wahudumu wanaofanya kazi ya kupanga na kusambaza tembe hizo iliwaamuru kusitisha mradi huo maramoja punde tu rais Trump alipochukua hatamu za uongozi.

Hii ni dalili ya kutamatisha mradi wa PEPFAR ambao umekua nguzo muhimu kwa wananchi kutoka Washingdon mradi ambao umeokoa maisha ya raia wngi duniani.