YOUTUBER Diana Marua amezua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akimkabili mumewe Bahati Kioko kuhusu ni kwa nini aliacha kumdekeza kwa zawadi.
Wapenzi hao walikuwa wametembelea moja ya mashamba walioyonunua mwaka jana huko Ngong wakati Diana alimhoji Bahati kwa nini hataki kumwekea mradi katika shamba hilo ili kumuingizia faida.
Diana alisema kwamba Bahati amekuwa bahili katika siku za hivi karibuni kiasi kwamba hata hakumbuki ni lini mara ya mwisho alimpa zawadi.
Alimkabili akitaka kujua nini kilibadilika akaacha kumdekeza kwa zawadi, na kuhoji iwapo mumewe alifilisika.
“Mimi nataka mali kila mahali, wewe hakikisha tu ninapata mali ndio mwisho wa siku ninatengeneza faida kutokana na hiyo mali. Sikiliza, umechoka kunitunuku zawadi? Umesota?” Diana alimkabili Bahati.
Bahati kwa kujitetea, alisema kwamba uchumi wa Kenya hauko vizuri vile na kwamba hakuna mtu ambaye Januari hii ako na pesa.
‘Hakuna mtu ambaye hajasota sasa hivi, na huu uchumi kuna mtu hajasota kweli?’ Bahati alisema akimjibu mkewe.
“Hivyo tuseme hutaki kuni’surprise? Kusema tu ukweli ni lini mara ya mwisho ilini’surprise? Ni lini mara ya mwisho ulisimamisha Kenya kwa kunizawidi?” Diana alimuuliza tena.
Mama huyo wa watoto 3 alisema kwamba zawadi ya mwisho alipokea kutoka kwa mumewe ni gari aina ya Range Rover.
“Haujanipa surprise nyingine yoyote. Zawadi ya mwisho ambayo ilinipa ni Range Rover.Hujanizawidi tena, hujashughulika tena na mimi…na unajua mimi ni Mjaluo…” Diana alilalamika.
Kwa mujibu wa Diana, angetegemea Bahati angempa bonge la surprise kama kumweka kwenye mabango makubwa ya barabarani nchini kote.
Alisema kwamba Bahati sawa tu na wanaume wengine,
zawadi ghali na ya maana ambayo
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!