MTENGENEZAJI wa maudhui ya mitandaoni Terence Creative amevunja kimya chake baada ya zawadi ya gari dogo alilomnunulia mkewe kuwa gumzo la mitandaoni kwa baadhi ya mahasidi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Terence alisema kwamba walikotoka na mkewe ni mbali sana kiasi kwamba hawawezi kudharau chochote kidogo wanachobarikiwa nacho.
Mkuza maudhui huyo alisema kwamba anashangaa wanaolalamika kwamba gari alilomnunulia mkewe ni dogo wakati wengine wao hawana hata hiloc dogo.
Aliwasuta akisema kwamba yeye si sampuli ya watu wanaokomboa magari ya kifahari kuigiza kama wanawazawadi wapenzi wao na baadae kuyarudisha kwa wenyewe baada ya kutrend.
Terence alisema kwamba yeye haoni tatizo kwa zawadi hiyo kwani mkewe Milly Chwebby mwenyewe aliipokea kwa mikono miwili kwani anaelewa hapo ndipo uwezo wa mumewe ulifikia.
“We live to please God by doing good and impacting the society and teaching them to take the stairs ??sitakomboa Range Rover ni “gift” bibi yangu birthday ndio nitrend…that’s not we.Sitaki pressure,maisha mzuri ni kupeleka mambo mos mos na kujikuna unapofikia,hapa ndio uwezo wangu umenifikisha kwa sasa,polepole Mungu atazidi kutuneemesha kwa wakati wake,” Terence alisema.
Alirejelea maisha yake ya awali katika ndoa na kufichua kwamba kuna wakati walikuwa wanaomba hata kupata gari dogo bovu na Mungu akafungua milango yao.
Terence alisema kwamba zawadi hiyo ya gari dogo kwa mkewe ni ya umuhimu mkubwa kwani alishachoka kushuhudia mkewe akipapaswa makalio kwenye mlolongo wa kuabiri matatu.
“Nilitazama wanaume kadhaa wakimtukana mke wangu, wengine walimpapasa huku tukitumia njia za hadhara, nilipigana na kupigana mpaka nikachoka, nilimwomba Mungu anipe tu gari lolote ili niepuke fedheha kama hiyo,” alisema.
“Mungu alisikia na akajibu, alinijalia nauli ya teksi na sasa ametupatia gari (Nissan Note) tumesonga polepole mpaka mahali tuko saa hii. ?Tumejifunza kuthamini kupanda ngazi katika uwekezaji wetu wote na tuliapa kwamba hatutaishi juu ya uwezo wetu ili kuwafurahisha watu,” aliongeza.
Awali, mkewe aliwatolea uvivu watu waliokuwa wakikejeli gari alilopewa na mumewe kama zawadi akisema kuwa ni husda tu na chuki wanao.
“Mungu anajua jinsi @terencecreative na mimi tumetoka wapi. Mungu alitujalia, kwamba Mungu amemwezesha kuninunulia Toyota Vitz ni jambo kubwa sana kwangu/kwetu, kama unahisi vinginevyo sijutii rafiki yangu. Mahali Mungu ametutoa turuhusu kusherehekea hata hatua zetu ndogo,” Milly Chebby alifunguka.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!