
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Januari 29.
Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kilifi, Narok, na Kwale.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya barabara za Dagoretti na Kikuyu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Gongoni Salt Work na Malindi katika kaunti ya Kilifi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Seheu za maeneo ya Rotian, Kisiriri na Tipis katika kaunti ya Narok zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Shamu na viunga viake katika kaunti ya Kwale pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!