Taasisi ya wahandisi nchini IEK imetaka uteuzi wa aliyekuwa waziri wa jinsia Aisha Jumwa Katana utupiliwe mbali kama mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini,.

Katika taarifa yakeTaasisi ya wahandisi nchini IEK imetaka uteuzi wa aliyekuwa waziri wa jinsia Aisha Jumwa Katana utupiliwe mbali kama mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini,katika taarifa aliyotoa jana rais wa taasisi ya barabara nchini Shammah Kiteme alikariri kuwa uteuzi wa Aisha Jumwa uliotiwa katika gazeti la taifa la mnamo januari 7,2025 unakiuka ibara ya sheria ya taasisi na usimamizi wa barabara nchini.

Kiteme alieleza kuwa uteuzi huo hauafikiani na matakwa ya sheria ya bodi ya usimamizi wa barabara nchini chini ya kifungu nambari 7 cha 1999.

''Uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini jinsi ilivyonakiliwa katika gazei nambari 395 mnamo tarehe 17,2025 inaonyesha wazi kuwa nafasi hiyo haifai kuchukuliwa na afisa wa ngazi ya umma ambaye ana cheo serikalini kama Aisha Jumwa na vilevile akatilia doa mchakato uliotumika kumteua kwa kwangazia uanachama'' Bwana katana alieleza katika taarifa yake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

kulingana na sheria ya bodi ya usimamizi wa barabara nchini KRB uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa barabara ni sharti utoke ndani ya wanachama ambao wameteuliwa na mashirika maalumu matano,mashirika hayo ni  muungano wa wamiliki wa magari nchini(the  automobile association),taasisi ya wahandisi nchini (The institute of engineers of kenya),muungano wa wazalishaji bidhaa(The kenya associaion of manufacturer),taasisi  ya udhibiti na usimamizi wa mali ya umma(The institute of certified public accountants of kenya) na muungano wa usafiri nchini(The kenya transport association).

Bwana Kiteme alikariri kuwa sheria inakubali mtu ambaye  hashikilii wadhifa wa umma na tena ambaye ni mwanachama wa mashirika haya matano kwa uteuzi bora.

Bodi ya wahandisi inakariri kuwa mtu ndio awe na uwezo wa kusimamia bodi ya barabara nchini anasitahili awe amefanya kozi au ana ujuzi na ufahamu kuhusu masuala na ukarabati na udhibiti wa masuala yanayofungamana na uhandisi.

Bodi ya usimamizi wa barabara ndio ina jukumu la kuangalia hali za barabara nchini,kutoa ushauri jinsi ya kuunda na kukarabati barabara na kuhakikisha kuwa kila jambo linapangwa ipasavvyo.

Taasisi imerai na kuomba uteuzi mpya kufanywa ili kuwe na mtu ambaye ana udhibiti na ufahamu kuhusu masuala ya barabara kwa kufanya hivyo taasisi itakuwa na nguvu na mamlaka ya kutoa ushauri inavyofaa,kwa kuangazia hayo ilisemekana kuwa Aisha Jumwa hana ufahamu mkubwa kuhusiana na  masuala ya uhandisi.

Hata hivyo wito umetolewa wa kufutilia mbali uteuzi wa Bi Aisha Jumwa Katana kama mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa barabara  nchini  na badala yake mtu mwengine ateuliwe aitwae nafasi hiyo.