MBUNGE wa Likoni Mishi Mboko ameisifia bima mpya ya matibabu ya SHA akisema kwamba ina manufaa zaidi kuliko bima ya zamani ya NHIF.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Akizungumza katika mkutano mmoja kwenye video ambayo imekuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii, mbunge huyo kutoka pwani alisema kwamba manufaa mapya kwenye SHA yanastahili hongera na heko kwa rais William Ruto.


Mboko alisema kwamba kutokana na mazuri yanayokuja na SHA, anataka pia kuzaa mtoto wake wa mwisho na kumpa jina la rais William Ruto.


“Kina mama tutazaa ama hatuzai? Mimi pia nataka nizae mimba yangu ya mwisho nimtaje Dkt William Ruto. Ndio, nimtaje maanake SHA iko. Shida iko wapi kama kuna SHA?” Mboko alihoji.


Aliendelea kudadavua mazuri ambayo mpango huo mpya wa afya unawapa wananchi akisema kuwa hilo halimpi tatizo katika kutaka kupata mtoto mwingine tena.


“Kama nikizaa na kisu (siombi hilo) nalipiwa elfu 30 kwenda mbele, nikizaa kwa njia ya kawaida, nalipiwa shilingi elfu 10. Kitambo ilikuwa ni Sh2,500 na Sh5,000 kwa upasuaji, kisha bado tunataka kutia porojo na propaganda, jamaa wakati wa propaganda si sasa jamaa,” Mboko alieleza.


Sheria ya Afya ya Jamii (SHA), iliyotiwa saini na Rais Ruto kuwa sheria mnamo Oktoba 2024, inalenga kubadilisha Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) na kuweka mfumo mpana zaidi.


https://www.instagram.com/buzzroomkenya/reel/DFLYlUCS_xT/ 

Mpango huo mpya unatanguliza fedha nne ambazo ni: Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii, Mfuko wa Huduma ya Afya ya Msingi, Mfuko wa Dharura, Sugu na Ugonjwa Mgumu, na Mfuko wa Wakala wa Afya wa Kidijitali.


SHA imeundwa ili kuhakikisha ufikiaji wa huduma ya afya kwa wote, haswa kwa watu walio hatarini kama vile wanawake wajawazito, watoto, na familia zenye kipato cha chini.


Tofauti na NHIF, SHA inashughulikia huduma kama vile: uchunguzi wa hali za kawaida za afya kama vile saratani, vifaa vya usaidizi kwa wagonjwa walio na ulemavu wa kudumu, wa kimwili au wa hisia na matibabu ya dharura ikiwa ni pamoja na bima ya ufufuaji na uimarishaji wa hali mbaya.