Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


MKALI wa miziki ya Dancehall kutoka Jamaika, Konshens amefichua kwamba atarejea nchini Kenya kwa mara nyingine mwaka huu 2025 kama njia moja ya kikata kiu cha mashabiki wake.


Msanii huyo kupitia mitandao wake wa X, alichapisha sampuli ya maswali ambayo amekuwa akipokea kwenye DM zake kwa kusema kwamba asilimia 90 ya maswali hayo ni kuhusu ni lini atarudi Kenya.


Alisema ili kukata kiu cha mashabiki wake wa Kenya ambao wamekuwa wakimuulizia kwa muda mrefu, sasa ameamua atakuja Kenya japo hakubainisha ni lini.


Akiweka tagi kwenye picha ya skrini, hitmaker huyo wa ‘Turn Me On’ aliahidi kuwapamba mashabiki wake wa Kenya kwa uwepo wake mwaka huu, akisema ana mapenzi makubwa na nchi hii.


Mwimbaji huyo aliongeza kuwa ingawa mashabiki kutoka mataifa mengine pia wamekuwa wakimtumia ujumbe, Wakenya ndio waliotuma ujumbe mwingi zaidi, hivyo kumfanya akose chaguo ila kujibu.


Alibainisha kuwa jumbe zao ziliingia kila siku na kuwahakikishia hawana cha kuwa na wasiwasi nao, kwani bila shaka angewatembelea.


"Maswali 5 bora yanayoulizwa zaidi kwenye DM yangu kila siku. Ninaahidi 2025 bila shaka."


https://x.com/konshens/status/1882480619445243974 


Alipozuru nchini Kenya mwaka 2023, mkali huyo wa Dancehall alifichua kwamba ana mapenzi makubwa kwa taifa hili na hata kulitaja kama taifa-mama la pili kwake.


Msanii huyo alionyesha furaha yake kipindi hicho kwa kupewa jina la msimbo ‘Otieno’ ambalo alilikumbatia kwa fahari kubwa.


"Nuff love, Kenya, imekuwa kweli. Uhusiano wetu una nguvu zaidi kuliko hapo awali. Tukutane baada ya miaka 2/3, Konshens Otieno. #DANCEHALL,” mwimbaji huyo wa ‘Simple Blessings’ alitweet.