Mshawishi Maarufu kutoka nchini Brazil ameaga dunia kwenye meza ya oparesheni .

Ricardo Godoi alitaka kuwekea Tatoo kwenye mgongo wake wote. kwenye harakati hizo kama ilivyo adha alipewa dawa ambazo zilifaa kumusaidia wakati wa shughuli hiyo ila zikamletea mauti.

Godoi mwanaume wa miaka 45 alitekwa na Cardiac arrest baada ya kupokea dawa katika hospitali ya Dia Revitalite mjini Santa wakati ratiba ya kuwekewa Tatoo ilikua ikianza. Daktari walishindwa kurejesha uhai wake.

Ripoti kutoka kwa mmiliki wa studio iliyokuwa na majukuu ya kumuekea tatoo, alisema kwamba kilichotokea kilifanyika kabla ya kuanza shughuli ya kuweka tatoo.

"Kilichotendeka ni kwamba, mwanzo wa matibabu na kudungwa shindano, ndipo alipotekwa na ugonjwa wa Moyo. hilo lilitendeka kabla ya sahughuli nzima kuanza."

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Aliangaliwa kwa upesi na daktari anaeshugulikia matibabu ya dharua ya moyo akaja kujaribu kurejesha uhai wake ila hakufaulu."

"Godoi alikua anaenda kufanyiwa tatoo kwa mgongo wake wote na sisi alivyokua ametaka. Ili kufanikisha hili tulitafuta hospitali ya kibinafsi yenye vifaa vyote vinavyohitajika na madaktari wa kutosha pamoja na dawa zinazohitajika kwa ajili ya shughuli nzima.

Tulitafuta pia dakitari ambaye amehitimu kutusaidi kwa shughuli hio na stakabadhi zake ziliidhinishwa na hospitali".

'Vipimo vyote vikafanywa ikiwemo kupima damu na vipimo havikuonesha hatari yoyote ya kufanya shughuli hio, Ricardo akaweka sahihi  kwenye sitakabadhi ili tuendelee na shughuli hio." alieleza mmiliki wa kampuni ka kuchoora tatoo.

Kwenye mtandao wa Ricardo wa instagram kumeandikwa, " ni kwa machungu na kujutia tunawatangazia kuhusu kifo cha Ricardo Godoi kilichotokea Jana mchana, acha kumbukumbu zake zikumbukwe na heshima kwa wote waliomjua.

Kabla ya kifo chake alikua ameandika kwenye mtandao wake huo ambao una wafwasi zaidi ya 200,000 kwamba alikua anaenda kufanyiwa sajari na wangekutana baada ya muda mchache.

" Niko kwenda kufanyiwa oparesheni  na nitarudi hapa baada ya saa kumi jioni.

Ricardo Godoi amekua pia mwanabiashara mkubwa na kampuni ya kuuza magari ya sports.  'sports car'