Wizara ya Afya imetangaza uthibitisho wa wagonjwa watano wapya wa Mpox nchini.
Katika taarifa ya Jumatatu, Katibu Mkuu wa Afya ya Umma Mary Muriuki alisema kesi hizo ziliripotiwa katika kaunti za Kericho (kisa 1), na Taita Teveta (kisa 1) ambavyo viliripotiwa mnamo Januari 17, 2025.
Visa vya hivi punde zaidi ambavyo vilizoripotiwa Januari 21, 2025, ni Busia (visa 2) na Kilifi (kisa 1), alisema.
Jumla ya wagonjwa wa Mpox nchini sasa ni 36 kutoka katika kaunti 12.
Bi Muriuki alisema idadi kubwa zaidi ya visa vya ugonjwa huo vimeripotiwa katika kaunti ni Nakuru (visa 10), Mombasa (visa 8), na Busia (visa 3).
Kaunti zingine ambazo zimeripoti kesi ni Nairobi, Kajiado, Bungoma, Taita Taveta, Kericho, na Kilifi zenye visa viwili kila moja, pamoja na kisa kimoja kutoka Makueni, Kiambu na Uasin Gishu mtawalia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!