Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans



KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Januari 23.

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

 

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja  jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Nandi, Uasin Gishu, Bungoma, Kakamega, Embu, Kiambu,  na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Runda, Nothern Bypass na Runda Riviera zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kaboswa, Mbogo Valley, Kapchorua, na Siret katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kesses na Cheptiret katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Bungoma, sehemu za maeneo ya Chesamis na Kaptama zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Soko la Makunga katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Embu, eneo la Kui na soko la Gatitu zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Ngoigwa katika kaunti ya Kiambu litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Shimo la Tewa na Mtwapa katiika kaunti ya Mombasa pia yataathirika.